Matangazo

📢 IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA — KARIBU KWENYE BLOG RASMI   ✦   📰 UHAMIAJI HABARI BLOGU — TUNAKULETEA MATUKIO KILA SIKU   ✦   📲 FUATA IDARA YETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII   ✦   ✉️ WASILIANA NASI: info@immigration.go.tz   ✦   ☎️ +255-22-2850575/6

09 Mei 2019

Epuka Msongamano, Wahi sasa! #ePassport


UHAMIAJI YATOA ONYO KALI KWA MAWAKALA (VISHOKA) WANAOTUMIA VIBANDA VYA WAJASIRIAMALI VILIVYOPO MKABALA NA OFISI YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU KUWATAPELI WANANCHI.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hanelore Manyanga amekutana na wafanya biashara na wajasiriamali wanaofanya biashara katika mtaa wa Loliondo, Kurasini - Jijini Dar es salaam. Mtaa huo upo Mkabala na Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu na kuna shughuli mbalimbali za biashara ikiwamo Mamalishe, Mawakili, Wapiga picha (Passport size) pamoja na watoa huduma za Stationaries.

Kamishna Manyanga amewataka wafanya biashara hao kuisaidia Idara ya Uhamiaji kupiga vita mawakala wa huduma za Uhamiaji (Vishoka ambao wanawatapeli wananchi wanaohitaji huduma za Uhamiaji katika maeneo hayo.

“Kumekuwepo na wimbi la Matapeli wanaojifanya kuwa Maafisa Uhamiaji wanawatapeli Wananchi kwa kuchukua pesa zao na kuwaahidi kuwasaidia kupata huduma za Uhamiaji ikiwa ni pamoja na Pasipoti, Viza, na Hati za Ukaazi kwa haraka. Kupitia kikao hiki nawaagiza kuwa mfanye biashara kwa mujibu wa matakwa ya leseni zenu kama inatokea kuna mtu ambaye siyo mhusika au anatumia vibanda vyenu kuwatapeli wananchi, tafadhali toeni taarifa Uhamiaji” alisema Kamishna Hanelore Manyanga

Aidha, Kamishna Manyanga aliongeza kuwa Idara ya Uhamiaji imedhamiria kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wote wanaojifanya Maafisa Uhamiaji na kuwatapeli Wananchi.
Wakitoa maoni yao katika kikao hicho baadhi ya wajasiriamali hao wametoa maoni yao na kuonesha kuchukizwa na vitendo hivyo ambavyo vinafanywa na watu ambao siyo waadilifu na kuchafua taswira nzuri ya Idara ya Uhamiaji na biashara zao kwa ujumla.

“Ni jambo jema kualikwa hapa kujadili suala hili, hata sisi tumekuwa tukichukizwa na hawa watu lakini tunashindwa kutoa taarifa kwani hatujui tumwambie nani, unakuta mtu anakuja pale mgahawani na mtu wanasaidiana kujaza fomu za Uhamiaji na baadae wanaondoka. Kupitia kikao hiki sasa tutakuwa tunatoa taarifa Uhamiaji lakini tunaomba tukitoa taarifa hizo zifanyiwe kazi na pia taarifa hizo ziwe siri” alisema Bi. Praise

Kupitia Kikao hicho wafanya biashara hao kwa pamoja wameahidi kushirikiana na Idara ya Uhamiaji na kuwafichua Mawakala/Vishoka wanaotumia Ofisi za mawakili, stationeries na migahawa kufanyia shughuli za Uhamiaji ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa yeyote atakayejihushisha na kazi za Uhamiaji katika maeneo yao ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Pasipoti Gerald J. Kihinga, ametoa wito kwa Wananchi kuwa hakuna Uwakala katika huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji. Hivyo mtu anayeomba Pasipoti ya Tanzania au Vibali vya Ukaazi anatakiwa awasilishe maombi yake kupitia tofuti ya Idara ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni www.immigration.go.tz

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Pasipoti Gerald J. Kihinga, Kaimu Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Paul Eranga pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Peter G. Mbaku.

Bi. Praise akichangia hoja katika kikao hicho.


Bw. Mulokozi ambaye ni mjasiriamali katika moja ya vibanda vilivyo mkabala na Ofisi ya Uhamiaji akieleza utayari wake katika kukabiliana na tatizo la vishoka wakati wa kikao hicho






Kaimu Kamishna wa Usimaizi na Udhibiti wa Mipaka, naibu Kamishna Paul Eranga akiongea wakati wa kikao hicho


Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Kamishna Hannelore Manyanga akiongea wakati wa kikao hicho

Baadhi wa wafanyabiasha na wajasiriamali wanaofanya shughuli zao mkabala na jengo la Uhamiaji Makao Makuu Kurasini wakiwa katika kikao cha pamoja na Idara ya Uhamiaji ili kutafuta suluhu la Vishoka wanaotumia sehemu zao za biashara kama ofisi


Kamishna wa Uraia na Pasipoti, Kamishna Gerald Kihinga akiongea wakati wa kikao hicho


06 Aprili 2019

TANZANIA, ETHIOPIA NA KENYA ZAKUTANA KUTAFUTA SULUHISHO LA KUTATUA TATIZO LA WAHAMIAJI HARAMU NA KUIMARISHA USHIRIKIANO MIPAKANI


Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa  Ngazi ya juu wa Kikanda uliofanyika katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam kuanzia tarehe 02-04 April mwaka huu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na Wadau wa Maendeleo (Development Partners) ambao ni Balozi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Norway, Ubelgiji, EU, UN-RCO, na ICRC na kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Alphaxad Lugola ulilenga  kutafuta njia ya namna ya kukabiliana na ongezeko la wahamiaji haramu, wanaoingia kinyume cha sheria hapa nchini kupitia njia ya Kusini (Southern route).

Mkutano huo ulitanguliwa na mkutano wa  Wataalamu wa masuala ya uhamiaji kutoka nchi za Tanzania, Ethiopia na Kenya chini ya Uenyekiti wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.

Pamoja na mambo mengine nchi hizo zimeweka mikakati ya pamoja katika kushughulikia changamoto ya biashara haramu ya  binadamu (Human Trafficking & Smuggling) na usafirishaji kimagendo wa binadamu (Human Smuggling), kuangalia namna bora ya kubadilishana taarifa za Wasafirishaji (Traffickers & Smugglers) na mikakati ya kuwaondosha nchini wahamiaji haramu na kuhakikisha hawarejei tena nchini bila kufuata taratibu.

“Ni mkutano wenye nia njema kwa nchi yetu, kwani hapa tumekutana ili kuweka mikakati namna ya kudhibiti mfumo mzima wa biashara haramu ya binadamu na usafirishaji magendo ya binadamu kutoka pembe ya Afrika kupitia njia ya Kusini ambapo Tanzania ni sehemu ya hiyo njia. Majadiliano yameenda vyema na tutegemee matokeo mazuri. Kila nchi mwalikwa imeahidi kufanya juhudi katika kudhibiti tatizo hili” Alieleza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala.

Tanzania imekuwa ni njia ya Usafirishaji wa Magendo ya Binadamu kuelekea kusini mwa Afrika ambapo Idara ya Uhamiaji nchini kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba 2018 ilifanikiwa kuwamata na kuwachukulia hatua mbalimbali jumla ya wahamiaji haramu  1024 kutoka pembe ya Afrika wengi wao wakiwa raia wa Ethiopia.

Hatua mbalimbali za kudhibiti tatizo hili zimeendelea kuchukuliwa, tayari jumla ya wahamiaji haramu 583 kutoka Ethiopia waliomaliza adhabu ya kutumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini walirejeshwa nchini kwao katika kipindi cha mwaka jana.

Aidha katika kipindi hicho, vyombo vya usafiri 10 vilitaifishwa na Serikali baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu  kinyume cha Sheria za Uhamiaji.

“Tunaishia kuwakamata dereva wa Fuso anaepakia wahamiaji haramu, Tunataka madalali wenyewe wasakwe wakamatwe, Kwahiyo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji ndani ya mwezi mmoja angalau basi kwa uchache uje na orodha ya hawa madalali wawili watatu hata kama ntaambiwa kwamba  wako nchi nyingine ili tuweze kutumia sheria zilizopo kuweza kuwakamata na kuwarejesha nchini ili kumaliza huo mtandao” Aliagiza Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kangi Lugola.

Mkutano huu unategemea kuleta matokea chanya kwa Idara ya Uhamiaji katika suala zima la udhibiti wa wahamiaji haramu kwani ni wa kwanza kufanyika na kuwashirikisha wadau kutoka nchi za pembe ya Afrika ambako ndiko wahamiajii haramu wengi wanaokamatwa nchini hutokea pamoja na Washirika wa Maendeleo.