Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda Tanzania (TRITA), chini ya Idara ya Uhamiaji Tanzania, kinawaalika wataalamu na wadau wa taasisi za umma na binafsi kushiriki Warsha ya Mwaka ya Usimamizi wa Uhamiaji Tanzania 2026. Warsha itafanyika 18 hadi 20 Novemba 2026 katika Cate Hotel & Convention Centre, Morogoro.
Jukwaa hili litawakutanisha wanaoshughulika na rasilimali watu, sheria, mawasiliano, udahili, biashara na utalii ili kubadilishana uzoefu na kujadili usimamizi wa masuala ya uhamiaji na utoaji wa huduma bora.
Kaulimbiu ya warsha
“Usimamizi Endelevu wa Masuala ya Kiuhamiaji Nchini: Kukuza Ubunifu wa Kidijitali na Mifumo Jumuishi kwa Utoaji Huduma Bora.”
Majadiliano yataangazia ubunifu wa kidijitali, mifumo jumuishi na uratibu wa wadau katika huduma zinazohusisha wageni na uhamiaji nchini. Washiriki watapata nafasi ya kuongeza maarifa, kujenga mitandao ya kitaaluma na kujadili changamoto na mbinu za kuzitatua.
Nani anaalikwa?
Waratibu na wasimamizi wa rasilimali watu (HR), mawakili na wanasheria, maafisa habari na uhusiano wa umma, maafisa uhusiano, maafisa udahili, wamiliki wa biashara, waendeshaji wa utalii, pamoja na wadau wengine kutoka sekta za umma na binafsi wanaohusika na masuala ya wageni na usimamizi wa uhamiaji.
Taarifa za ushiriki
Tarehe: 18–20 Novemba 2026
Mahali: Cate Hotel & Convention Centre, Morogoro
Ada: TSh 1,000,000 kwa mshiriki
Jisajili kwa kuskani QR code iliyopo kwenye poster rasmi ya warsha hapa chini. Kwa ufafanuzi wa usajili na malipo, wasiliana moja kwa moja na TRITA kabla ya kufanya malipo.
Mawasiliano: +255 795 267 160 | info@trita.ac.tz
TRITA inawaalika wadau kutumia fursa hii kuimarisha uelewa na ushirikiano wa kitaaluma katika usimamizi endelevu wa uhamiaji.