Dar
es salaam, Tanzania
Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala ameongoza mamia ya watu katika Ibada
takatifu ya kumuaga mtumishi wa Idara ya Uhamiaji aliyekuwa Katika Kitengo cha
Uhasibu Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma Marehemu Geofrey Hubert Saria.
Ibada hiyo imefanyika jana katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT
DMP) Tabata Chang’ombe ambapo ilihudhuriwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dkt. Anna Makakala, Kamishna wa uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogelo,
Kamishna wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga na Kamishna wa Vibali vya Ukaazi
Visa na Pasi Mary Palmer (ndc).
Wengine
waliohudhuria Ibada hiyo ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna
Msaidizi (ACI) Edmund Mrosso Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania
Mrakibu Paul Mselle Maafisa, Askari na Watumishi Raia wa Uhamiaji sanjari na ndugu na jamaa wa
marehemu Saria.
Akiongea na
Maofisa, Askari, Wtumumishi Raia ndugu na jamaa wa Marehemu wakiwemo Waumini wa KKKT Waliohudhuria Ibada hiyo CGI
Dkt. Makakala amesema kwamba marehemu
alikuwa mchapakazi katika kutekeleza majukumu yake kwa utii uhodari na weledi
wa hali ya juu wakati wote huku akionesha ushirikiano na wafanyakazi wenzake.
“Marehemu
Saria amefariki katika kipindi ambacho Idara Idara ya Uhamiaji bado inamhitaji
sana kwa mchango wake katika Kulitumikia Taifa”
alisema CGI Dkt. Makakala
Akisoma Wasifu wa
Marehemu Mrakibu wa Uhamiaji Andrew Malyeta alisema Marehemu Geofrey Saria
alizaliwa 25 Octoba 1989 katika
Hospitali ya Mikocheni katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Mwaka 1997 Marehemu
alipata Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Tabata Relini iliyoko Jijini Dar
e salaam na kuhitimu mwaka 2003, Mnamo mwaka 2004 alijiunga na Shule ya
Sekondari Makongo iliyoko Jijini Dar es salaam na Kuhitimu kidato cha nne mwaka 2007.
Aidha mwaka 2008
alirudi tena katika shule ya Sekondari Makongo kwa masomo ya Kidato cha Tano na
Sita na kuhitimu mwaka 2010, mwaka 2011 marehemu alijiunga na chuo cha Uhasibu
Arusha kwa Masomo ya Elimu ya Juu na mwaka 2013 alihitimu na kutunukiwa
shahada ya kwanza ya Uhasibu.
Mwaka 2014 Marehemu
alifanya Mtihani wa Uhasibu na Kutunukiwa cheti cha juu cha Uhasibu CPA (T) na
Bodi ya Taifa ya Uhasibu Tanzania (NBAA).
Marehemu Saria
Aliajiriwa serikalini katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ndani ya Idara ya
Uhamiaji kuanzia tarehe 01 Septemba 2015 akiwa Mhasibu daraja la II na alipangiwa Kituo cha Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dar e s salaam.
Mnamo Tarehe 19 Oktoba Marehemu alihamishwa kutoka katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam na kuhamia Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma, kufuatia uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma.
Mpaka umauti unamkuta marehemu alikuwa akihudumu katika Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma Kitengo cha Uhasibu.
Marehemu alifariki siku Jumapili ya tarehe 23 Agosti mwaka huu 2020 kwa ajali ya gari iliyotokea Mkoani Morogoro alipokuwa safarini kutka Dar es salaam kuelekea Dodoma
Marehemu alizaliwa 25 Ocktoba 1989 na Kufariki Tarehe 23 Agosti 2020 kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Dar es salaam.
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa salamu za mwisho kwa marehemu Geofrey Saria |
|
Mwili wa Marehemu ukiwasili Kanisani
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiteta jambo na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogelo |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiteta jambo na Kamishna wa Urai na Pasipoti Gerald Kihinga |
|
Mtunza Nidhamu wa Idara ya Uhamiaji RSM Zahara Akida akifuatilia kwa Makini Mahubiri katika Ibada ya Kumuaga marehemu Geofrey Saria katika Kanisa la KKKT DMP Usharika wa Tabata
|
|
Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya Ukaazi Pasi na Visa Mary Plmer (Ndc) Kulia akiteta jambo na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Edmund Mrosso wakati wa Ibada ya Kuuaga Mwili wa Marehemu Geofrey Saria
|
|
Pichani wa Kwanza Kulia ni Mama Mzazi wa Geofrey Saria akiwa katika Ibada ya Kumuaga Mwanae katika Kanisa la KKKT Tabata
|
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa salamu za rambi rambi wakati wa ibada ya Kumuaga Marehemu Geofrey Saria |
|
Familia ya Marehemu Geofrey Saria Ikitoa Salamu zao za Mwisho
|
|
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mrosso akitoa salamu za mwisho kwa marehemu Geofrey Saria |
|
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzani Mrakibu Paul Mselle Akitoa Salamu za Mwisho kwa Marehemu Geofrey Saria
|
|
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika msibani
|
|
Makaburini |
|
Makamishna wa Uhamiaji wakiweka shada la Maua
|
|
Mama Mzazi wa Marehemu na ndugu wa Karibu wakiweka Shada la maua |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mchungaji wa KKKT DMP Usharika wa Tabata aliyeongoza Ibada ya kumuaga Marehemu Geofrey Saria |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akimpa pole na kuagana na Mama Mzazi wa Marehemu Geofrey Saria |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiagana na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Edward Chogelo |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiondoka mara baada ya Kuhudhuria Ibada Takataifu na Mazishi ya Marehemu Geofrey Saria (Picha Zote na Kitengo cha Uhusiano
|
Uhamiaji Makao Makuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni