Dar es salaam
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala ameshiriki hafla ya gwaride la heshima la kumuaga Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu na Kamishna Mstaafu wa Polisi aliyesimamia Masuala ya Fedha na Lojistiki (CP) Leonard Paul Lwabulaza katika uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini Jijini Dar es salaam.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Christopher Kadio sanjari na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama nchini vikiongozwa na Mkuu wa Majeshi (CDF)Jenerali Venance Mabeyo.
Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya hafla hiyo (IGP) Mstaafu Balozi Ernest Mangu ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kumuamini kwa kipindi chote cha uongozi wake kutimiza majukumu yake ya kulingoza Jeshi la Polisi kwa utii uhodari na weledi wa hali ya juu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amesema anamskukuru sana IGP Mstaafu Mangu kwani wakati wa uongozi wake alijifunza mengi ambayo sasa yanamsaidia katika kuliongoza Jeshi hilo.
IGP Mstaafu Balozi Ernest Mangu alizaliwa tarehe 25 Agosti 1960 katika kijiji cha Majengo kata ya Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida.
Alijiunga na Jeshi la Polisi mnamo tarehe 01 Juni 1983 na Kupata cheo cha Konstebo wa Polisi mwenye namba D.2676 na kupangiwa kazi (GD) Katika Kituo cha Polisi Oysterbey Kinondoni Dar es salaam
Aidha IGP Mstaafu Balozi Mangu Alipata Elimu ya Msingi katika Shule Msingi Kinyagigi Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida mwaka 1971-1977, na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Tumaini iliyopo eneo la Kinampanda Wilaya ya Iramba Mkoani Singida kuanzia Mwaka 1978-1981.
Mwaka 1986-1987 alisomea astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Mwaka 1988-1992 alihitimi Shahada ya kwanza ya sheria LLB (Hons) katika Chuo kikuu cha DSM (UDSM), Aidha mwaka 2006-2007 alihitimu stashahada ya Uzamili katika usimamizi wa Rasilimali kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es salaam na mwaka 2004 hadi 2010 alihitimu shahada ya uzamili katika masuala ya Usalama kwenye chuo International Security Affairs National Defence University Washington DC Marekani.
IGP Mstaafu Balozi Mangu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo kuwa Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dodoma, baadae kuwa Msaidizi Binafsi (PA) wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), pia aliwahi kuwa Msaidizi Binafsi (PA) wa Inspeketa Jenerali wa Polisi (IGP).
Aidha IGP Mstaafu Mangu amewahi pia kuwa Kamnda wa polisi Mkoa (RPC) katika Mikoa ya Pwani, na Mwanza na Baadae kuwa Mkurugenzi wa Intelejensia wa Jinai hadi hapo alipopandishwa cheo kuwa IGP.
Mwaka 2014 IGP Mstaafu Balozi Mangu alipandishwa cheo kutoka kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Oktoba 26 Mwaka 2017 alistaafu Utumishi Katika Jeshi la Polisi na Kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda.
IGP Mstaafu Balozi Mangu amewahi kutunukiwa Nishani Mbalimbali zikiwemo za Utumishi wa muda mrefu na tabia njema, Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu, Nishani ya Mwenge wa Uhuru na Nishani Iliyotukuka.
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akiwasili katika uwanja wa Chuo cha Polisi Dar es salaam kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro
|
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akipokea Salamu ya HeshimakutokaKtika Gwaride Maalumu la Kumuaga |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akikagua Gwaride |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akikagua Brass Band ya Jeshi laPolisi |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akisalimiana na Kuagana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akisalimiana na Kuagana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akiwaga Maofisa na Askari wa Polisi |
|
Inspekta Jenerali (Mstaafu) wa Jeshi la Polisi nchini Balozi Ernest Jumbe Mangu akisindikizwa kutoka nje ya Geti kama ishara ya mwisho wa Utumishi wake katika Jeshi la Polisi |
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Christopher Kadio |
|
Kamishna (Mstaafu) wa Polisi aliyesimamia Masuala ya Fedha na Lojistiki (CP) Leonard Paul Lwabulaza akiwasili |
|
Kamishna Mstaafu wa Polisi aliyesimamia Masuala ya Fedha na Lojistiki (CP) Leonard Paul Lwabulaza akikagua Gwaride |
|
Kamishna Mstaafu wa Polisi aliyesimamia Masuala ya Fedha na Lojistiki (CP) Leonard Paul Lwabulaza akiwaaga Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi |
|
Picha ya Pamoja na Familia ya IGP Mstaafu Balozi Ernest Mangu |
|
Picha ya pamoja na familia ya Kamishna Mstaafu wa Polisi aliyesimamia Masuala ya Fedha na Lojistiki (CP) Leonard Paul Lwabulaza |
|
IGP Mstaafu Balozi Ernest Mangu akiongea na Waandishi wa Habari (Picha zote na Kitengo cha Habari na Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni