Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Oktoba 2017

UHAMIAJI WAFANYA USAFI NA KUFARIJI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala aliongoza watumishi wa idara hiyo kwenye zoezi la usafi na kuwafariji wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke.
Zoezi hilo lililofanyika leo jumamosi ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali la kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. 


Baada ya kukamilisha zoezi la usafi, Dkt. Makakala akiongozwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Temeke Dkt. Amaani K. Malima walielekea katika wodi ya watoto na wodi ya kina mama wajawazito na kugawa vifaa na zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafariji wagonjwa hao.

Aidha, Dkt. Makakala alikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa uongozi wa hospitali kwa ajili ya kuimarisha afya na usafi hospitalini hapo.


Vifaa na zawadi mbalimbali zilizogawiwa kwa wagonjwa hospitalini hapo zilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi milioni nane.