Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

03 Machi 2025

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NAMBA 06 YA MWAKA 2024/2025.


 #UhamiajiUpDates 

Na. Konstebo Jafar Mshihiri, Mkinga Tanga.


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, (CI) Hassan Ali Hassan, jana tarehe 02 Machi 2025, akiwa mgeni rasmi, amefunga rasmi mafunzo ya Uongozi kwa Maafisa na Askari wa Uhamiaji 320 katika Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga, Mafunzo haya ni sehemu ya kozi namba 06 ya mwaka 2024/2025.

Katika hotuba yake, CI Hassan Ali Hassan aliwapongeza Maafisa na Askari waliohitimu mafunzo yao na kuwaasa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia majukumu ya Idara ya Uhamiaji ili kukuza nyanja mbalimbali za kiuchumi na usalama nchini. 

"Nyinyi ni nguzo muhimu katika utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji, hivyo ni lazima kuonesha ufanisi, uadilifu na weledi mkubwa kwa ustawi wa usalama wa mipaka ya Nchi yetu,” alisema Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar CI Hassan A. Hassan.

Vilevile, Kamishna Hassan A. Hassan aliipongeza Brass Band ya Uhamiaji, ambayo kwa mara ya kwanza iliongoza Gwaride katika hafla ya kufunga mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uhamiaji Raphael Kubaga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Charles Obado ameishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mafunzo ya Promosheni Kozi kwa Maafisa na Askari sanjari na kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo utekelezaji wa mradi wa nyumba 12 za makazi ya wakufunzi  ambao unaendelea chuoni hapo na ukikamilika utaenda kusaidia kuboresha makazi ya wakufunzi pamoja na familiya zao kwa faida ya sasa na baadae.

Aidha amemshukuru pia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala kwa uongozi wake uliotukuka, kwani maelekezo yake na maono yake juu ya chuo hicho yanapelekea mafanikio makubwa ya Idara ya Uhamiaji na Tanzania kwa ujumla.

Mafunzo hayo yaliyojumuisha Maafisa na Askari 320 kutoka Tanzania bara na Zanzibar yalifunguliwa rasmi tarehe 14 Desemba 2024 na kuhitimishwa Jana tarehe 02 Machi 2025 huku yakilenga kuboresha uongozi na utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji na Taifa kwa ujumla.




Kikundi cha Bendera


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, (CI) Hassan Ali Hassan, Akiwasili uwanja wa Paredi wa Dk. Anna P. Makakala kufunga mafunzo ya kozi ya Uongozi namba 5/2025

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, (CI) Hassan Ali Hassan, Akipokea salamu ya heshima Aliwasili uwanja wa Paredi wa Dk. Anna P. Makakala wakati wa kufunga mafunzo ya kozi ya Uongozi namba 5/2025

Brass Band ya Idara ya Uhamiaji



Gwaride la Wahitimu (Gadi ya Wanaume) wa Kozi ya Uongozi namba 5/2025 Wakipita mbele kwa   mwendo wa pole.



Gwaride la Wahitimu (Gadi ya Wanawake) wa Kozi ya Uongozi namba 5/2025 Wakipita mbele kwa mwendo wa haraka.








Mkuu wa Chuo Cha Uhamiaji Raphael Kubaga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Charles Obado


#MjueJiraniYako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni