#UhamiajiUpDates Na. Konstebo Robert Ngowi, Tukuyu-Mbeya.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (ACI) Filbert Ndege, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ameongoza Mazishi ya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Amon Oscar Mogha, ambayo yamefanyika leo tarehe 01/03/2025, katika Kijiji cha Kayuki, Tukuyu, Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Amon Mogha alikuwa Afisa utumishi katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Dodoma, alifikwa na umauti ghafla jioni ya tarehe 25/02/2025, maeneo ya Chidachi, Jijini Dodoma, akiwa njiani anatoka mazoezini.
Aidha, mwili wake uliagwa Jana tarehe 28 Februari 2025 Jijini Dodoma na kusafirishwa hadi nyumbani kwao Kijiji cha Kayuki, Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ambapo amezikwa kwa heshima na Maafisa na Askari wa Uhamiaji, familia, ndugu, na jamaa.
Akitoa salamu za Uhamiaji kwa niaba ya CGI Dkt. Anna Makakala Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya ACI alisema Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, ametoa pole kwa familia ya Marehemu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake wa Idara ya Uhamiaji kwa msiba huo mzito.
ACI Ndege ameongeza kwamba CGI Dkt. Makakala amesema kuwa Marehemu Amon Oscar Mogha alijitolea kwa ufanisi katika kutekeleza majukumu yake ya uhamiaji, na atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika Idara ya Uhamiaji. Aidha alisisitiza umuhimu wa kuenzi na kuendelea na kazi nzuri aliyoiendeleza Marehemu, akiashiria jitihada za timu ya Uhamiaji katika kutimiza majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa umma sanjari na kudumisha Kauli mbiu ya Uhamiaji "Upendo, Mshikamano Uwajibikaji na kukataaa Rushwa .
Marehemu SSI Amon Mogha alizaliwa tarehe 03 Septemba 1979 Tukuyu, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya na kusoma shule na vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi, mpaka anaajiriwa na Idara ya Uhamiaji Mwaka 2007.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Amon Oscar Mogha atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka na wa kujitolea na kwa faida ya Idara ya Uhamiaji na Taifa kwa ujumla kwa Manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni