Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

26 Machi 2018

ANATAFUTWA


NDG. FAISALI HIRARY MWENYE PICHA HAPO JUU ANATAFUTWA NA IDARA YA UHAMIAJI KWA KOSA LA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU KINYUME NA KIFUNGU CHA 46 CHA SHERIA YA UHAMIAJI, SURA YA 54, REJEO LA MWAKA 2016.

YEYOTE MWENYE TAARIFA KUHUSU MTUHUMIWA HUYO, ANAOMBWA KUIFIKISHA KATIKA OFISI YOYOTE YA UHAMIAJI AU KITUO CHA POLISI KILICHO KARIBU NAYE.

AIDHA, TAARIFA INAWEZA KUTOLEWA KWA NJIA YA SIMU KUPITIA NAMBA IFUATAYO: 0768 636 505.


Pamoja Tushirikiane Kuilinda Nchi Yetu

-------------------------
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA UHUSIANO,
IDARA YA UHAMIAJI,
 MAKAO MAKUU,



07 Machi 2018

ELIMU KWA UMMA SINGIDA YAZAA MATUNDA, WATUHUMIWA SITA WAKAMATWA

Idara ya Uhamiaji Mkoani Singida imetoa elimu kwa Umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji zikiwemo Pasipoti, Vibali vya Ukaazi,Uraia na Uhamiaji haramu. Zoezi hilo linaendelea kufanyika katika Wilaya zote Sita za mkoa wa  Singida ambazo ni Manyoni, Mkalama, Ikungi, Iramba, Singida Mjini na Vijijini.  

Katika kutekelaza zoezi hilo Maafisa Uhamiaji Wilaya wanashirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya husika pamoja Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa/Vitongoji mbalimbali ikiwa ni lengo la kuwajengea uelewa Viongozi hao kuhusu masuala yanayohusu Uhamiaji.

Sambamba na elimu kwa umma, Uhamiaji Singida wameimarisha Mapambano ya Wahamiaji haramu kwa kufanya misako na doria za mara kwa mara katika maeneo yanayozaniwa kuwa hifadhi ya Wahamiaji haramu.

“Mpango huu wa Elimu kwa Umma umesaidia kufanikisha kuwakamata Wahamiaji haramu [02] Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania [04] ambao wanajihusisha na biashara haramu ya kusafirisha Wahamiaji haramu, Watuhumiwa wote wamefikishwa Mahakamani. Wananchi wamekuwa na mwamko na wamesaidia katika kuwaafichua watuhumiwa hao.  Natoa rai kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamaji kwa kutoa taarifa kwa Vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapobaini kuna mtu au kikundi cha watu wanaodhaniwa kuwa wahamiaji haramu’’ alizungumza Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa Singida, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Angela M. Shija.

Katika zoezi hilo kwa Wilaya ya Iramba inaongozwa na Kaimu Afisa Uhamiaji Wilaya Mkaguzi Dotto Selasini na kwa Wilaya za Singida Mjini na Vijijini linaratibiwa na kusimamiwa na Wakaguzi Wasaidizi Lawi Kumburu na Marcelin Marwa. Fuatilia habari picha zifuatazo:-











Kaimu Afisa Uhamiaji (W) Iramba Mkaguzi wa Uhamiaji Dotto Roman Selasini akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Kidaru katika Tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba, katika muendelezo wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Singida kutoa elimu kwa Umma


Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Lwehaula (aliyeshika kitabu) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya katika mkutano ambapo Kaimu Afisa Uhamiaji alipata fursa ya kutoa elimu kwa Umma.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kidaru waliohudhuria mkutano ambapo walipata elimu katika masuala mbalimbali yanasimamiwa na Idara ya Uhamiaji.


Wanakijiji wa Kidatu wakifuatilia kwa makini Elimu juu wa Wahamiaji Haramu iliyokuwa ikitolewa na Mkaguzi wa Uhamiaji Dotto Selasini




Wakaguzi wasaidizi wa Uhamiaji (kutoka kushoto) Lawi Kumburu na Marcelin Marwa wakitoa Elimu kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa Kata ya Minga (Singida Mjini) namna ya kuwatambua wahamiaji Haramu katika maeneo yao. Lengo kuu la kikao hicho ni kubadilishana uzoefu na kutoa elimu ya masuala ya uhamiaji katika mkoa wa Singida.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Marcelin Hanson  akifafanua jambo katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa Kata Minga na Maafisa Uhamiaji mkoa wa Singida lengo ni kupeana uzoefu na elimu katika masuala mbalimbali ya uhamiaji hasa tatizo la udhibiti wa Wahamiaji Haramu

Mtendaji wa Mtaa wa mtaa wa Arusha Road  Kata ya Minga Bw. Saidi Shabani akiuliza swali katika kikao cha kubadilishana uzoefu na uelimishaji wa masuala ya uhamiaji baina ya watendaji wa serikali za mitaa na maaisa Uhamiaji Mkoa wa Singida 

Mkaguzi wa Uhamiaji Lawi Kumburu akijibu swali kutoka kwa mmoja wa washiriki wa kikao cha kubadilishana uzoefu na uelimishaji wa masuala mbalimbali ya kiuhamiaji kwa watendaji wa serikali za mitaa na maafisa uhamiaji









06 Machi 2018

Uhamiaji walipotia 'Mguu' Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala cha jijini Dar

Ukaguzi wa uhalali wa Ukaazi wa watumishi wa chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala uliofanywa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiwa na Mheshimiwa Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako chuoni hapo Gongolamboto jijini Dar es salaam.