Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Julai 2020

Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Vyashiriki Kikamilifu Mazishi ya Hayati Mhe. Benjamin Mkapa

Lupaso, Mtwara

Vyombo vya ulinzi na Usalama Nchini Tanzania mapema wiki hii vimeshiriki Kikamilifu Mazishi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

Mazishi hayo yaliongozwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwemo ndugu na jamaa wa Hayati Benjamin Mkapa.

Mazishi hayo yalienda sambamba na Paredi ya heshima na upigaji wa mizinga 21 iliyoongozwa na Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.

Mkuu wa Majeshi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo aliwaongoza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini akiwemo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala katika kuweka mashada ya maua na kuweka udongo ndani ya kaburi la Hayati Mkapa.

Hayati Mhe. Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizaliwa Mwaka 1938 katika Kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na kufariki Julai 2020.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika eneo la Mazishi

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika eneo la Mazishi ya Hayati Bemjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso

Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogelo akiwa na Kamishana wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya ukaazi, Visa na Pasi Mary Palmer wakiwasili katika eneo la Mazishi kijijini Lupaso nyumbani kwa Hayati Mzee Mkapa

Kaburi likiwa katika hatua za mwisho kuandaliwa



Baadhi ya Viongozi wastaafu wakiwasili eneo la Tukio huku wakiongozwa na wataalamu wa Itifaki


Baadhi ya maofisa Askari na Raia wakitoa salamau zao za heshima za mwisho kabla ya kuuzika mwili wa Hayati Mzee Mkapa Nyumbani kwake Lupaso Mtwara



Maofisa Uhamiaji Mikoa ya Karibu nao Walihudhuria mazishi ya Hayati Mzee Mkapa


Waandishi wa Habari Mbalimbali nao waliweka Kambi Kijijini Lupaso-Mtwara ili Kuihabarisha Dunia  juu ya Tukio kubwa la Kitaifa la Mazishi ya Hayati Mzee Mkapa


Itifaki zikiendelea


Rais Dkt. John Pombe  Magufuli akihutubia Wanachi waliofika Kumuaga Hayati Mzee Mkapa Kijijini Lupaso Mkoani Mtwara
Gwaride la Mazishi likijiandaa kuingia Uwanjani 

Gwaride la Mazishi Likiingia Uwanjani




Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein akiweka Udongo katika kaburi la Hayati Mzee Mkapa

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania  (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akiwawakilisha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi  na Usalama Nchini Kuweka Udongo katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa



Familiya ya Hayati Mzee Mkapa ikiweka shada la Maua katika Kaburi lake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwaongoza Marais Wastaafu katika kuweka shada ya Maua katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa



Baadhi ya Mawaziri nao wakiweka shada la Maua


Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini wakiweka Mashada ya Maua katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiagana na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Kumaliza Shughuli ya Mazishi





Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Akiagana na Waku wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Mara baada ya Kumaliza Mazishi






(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)


Waziri Simbachawene Amzungumzia Hayati Mhe.Benjamin William Mkapa

Majeshi ya Tanzania yalivyomuaga Hayati Mzee Benjamin William Mkapa

27 Julai 2020

Buriani Rais Mstaafu Hayati Benjamini William Mkapa 1938-2020 Uhamiaji Tunakulilia, Pumzika kwa Amani

Idara ya Uhamiaji Tanzania Imeshiriki katika Kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe.  Benjamin William Mkapa Katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  jana alihudhuria Ibada ya Kumuaga Hayati Mzee Mkapa 

Aidha Viongozi wengine akiwemo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala alihudhuria pia ibada hiyo, pia viongozi wa serikali, Majeshi mbalimbali na Wananchi waliendelea kumuaga Hayati Mzee Mkapa.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Mwili wa Hayati Mzee Mkapa ukiwasili katika Uwanja wa Uhuru










 
Kamishna Jenerali w aUhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala akitoka Uwanjani Mara baada ya Kumaliza Misa Takatifu ya Kumuaga Hayati Mzee Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam






Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene alivyowasili kuuaga Mwili wa Hayati Mzee Mkapa







Baadhi ya Makamishna wa Uhamiaji Wakisubiri Taratibu za Kuaga Mwili wa Hayati Mzee Mkapa



Baadhi ya Maofisa Uhamiaji wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru tayari kwa Kuaga Mwili wa Hayati Mzee Mkapa










Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi akiwasili katika Uwanja wa Uhuru Kuaga Mwili wa Hayati Benjamin Mkapa



(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)