Lupaso, Mtwara
Vyombo vya ulinzi na Usalama Nchini Tanzania mapema wiki hii vimeshiriki Kikamilifu Mazishi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mazishi hayo yaliongozwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwemo ndugu na jamaa wa Hayati Benjamin Mkapa.
Mazishi hayo yalienda sambamba na Paredi ya heshima na upigaji wa mizinga 21 iliyoongozwa na Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.
Mkuu wa Majeshi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo aliwaongoza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini akiwemo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala katika kuweka mashada ya maua na kuweka udongo ndani ya kaburi la Hayati Mkapa.
Hayati Mhe. Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizaliwa Mwaka 1938 katika Kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na kufariki Julai 2020.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika eneo la Mazishi |
Kaburi likiwa katika hatua za mwisho kuandaliwa |
Baadhi ya Viongozi wastaafu wakiwasili eneo la Tukio huku wakiongozwa na wataalamu wa Itifaki |
Baadhi ya maofisa Askari na Raia wakitoa salamau zao za heshima za mwisho kabla ya kuuzika mwili wa Hayati Mzee Mkapa Nyumbani kwake Lupaso Mtwara |
Maofisa Uhamiaji Mikoa ya Karibu nao Walihudhuria mazishi ya Hayati Mzee Mkapa |
Waandishi wa Habari Mbalimbali nao waliweka Kambi Kijijini Lupaso-Mtwara ili Kuihabarisha Dunia juu ya Tukio kubwa la Kitaifa la Mazishi ya Hayati Mzee Mkapa |
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wanachi waliofika Kumuaga Hayati Mzee Mkapa Kijijini Lupaso Mkoani Mtwara |
Gwaride la Mazishi Likiingia Uwanjani |
Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein akiweka Udongo katika kaburi la Hayati Mzee Mkapa |
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akiwawakilisha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Kuweka Udongo katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa |
Familiya ya Hayati Mzee Mkapa ikiweka shada la Maua katika Kaburi lake |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwaongoza Marais Wastaafu katika kuweka shada ya Maua katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa |
Baadhi ya Mawaziri nao wakiweka shada la Maua |
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini wakiweka Mashada ya Maua katika Kaburi la Hayati Mzee Mkapa |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiagana na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Kumaliza Shughuli ya Mazishi |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Akiagana na Waku wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Mara baada ya Kumaliza Mazishi |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni