Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

07 Februari 2018

HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (MTANDAO).


HATUA ZA UJAZAJI FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (MTANDAO).

1.   INGIA KATIKA TOVUTI YA IDARA: www.immigration.go.tz KISHA NENDA KATIKA KITUFE CHA e-SERVICES
2.   CHAGUA PASSPORT APPLICATION FORM;
3.   CHAGUA OMBI JIPYA;
4.   TIKI KIBOKSI KUKUBALIANA NA MAELEKEZO;
5.   JAZA TAARIFA ZAKO KWA UKAMILIFU UKIFUATA MAELEKEZO NA MPANGILIO (FORMAT) KATIKA KILA KIPENGELE;
NB:
BAADA YA MWOMBAJI KUKAMILISHA KUJAZA TAARIFA ZAKE, ATAFAHAMISHWA YA KWAMBA USAJILI UMEKAMILIKA NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI, AMBAYO NI MUHIMU AIANDIKE PEMBENI NA KUIHIFADHI KWA KUMBUKUMBU ZA BAADAE. KISHA ATAPEWA NAMBA YA KUMBUKUMBU YA MALIPO (CONTROL NUMBER) NA KUTAKIWA KWENDA KULIPIA MALIPO YA AWALI (ADVANCE FEE) YA TSH 20,000.

BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI, NA KUPATIWA NAMBA YA OMBI NA NAMBA YA KUMBUKUMBU (CONTROL NUMBER), UKURASA UTAONEKANA KAMA IFUATAVYO:
INGIA KWENYE MENU YA M-PESA/TIGOPESA (*150*00#/*150*01#)
1. Bonyeza Namba 4 (Lipa kwa M-Pesa) - VODA
2. Bonyeza Namba 4 (Kulipia Bili) - TIGO
Kisha Weka/Ingiza Namba ya Kampuni
3. Ingiza Namba (888999)
4. Ingiza kumbukumbu Namba(Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….)
5. Ingiza kiasi (kama ulivyo elekezwa Mfano: 20,000 nk.)
6. Utapata Maelezo kuwa unalipa pesa NMB
7. Ingiza Namba ya Siri
8. Hakiki
9. Utapata Meseji toka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika;

Utapata meseji kutoka kwenye mfumo Namba 15200
kama muamala umekubalika;

10.       Mteja atatakiwa kurudi katika OMBI LINALOENDELEA:
11.       Kisha ataingiza NAMBA YA OMBI/SIMU na NAMBA YA RISITI

Na hapo ataweza kupakua Fomu yake ya Maombi
Ataiwasilisha Fomu hiyo katika Ofisi ya Uhamiaji Makao makuu au Afisi Kuu Zanzibar
1.  Jaza fomu ya malipo ya kielectroniki;
    2. Fuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu;
    3. Utapata meseji toka benki;
           Utapata meseji toka kwenye mfumo Namba 15200  
     kama muamala umekubalika.

Maoni 9 :

 1. utaratibu ni mzuri sana ila kwa maeneo yasiyokuwa na mtandao au hawana compyuta watafanyaje?haswa vijijini

  JibuFuta
 2. Ni mzuri ila sina hakika na bei ya passport kwa sasa. ni 20,000 au ni 150,000?

  JibuFuta
 3. ni utaratibu usio na ubabaishaji jee hiyo pesa 20000 ni kwa ajili ya paspot au ni kwa ajili ya malipo ya fom?

  JibuFuta
 4. Je mualikaj akiwa hana residence permit anaweza kutuma mkataba wa nyumba

  JibuFuta
 5. Kama kuna sehemu ukisahau kukamilisha majina unaweza kuiita form na kujaza ili kukamilisha majina matatu?

  JibuFuta
 6. its good thing but how are we going to send this form to immigration office?

  JibuFuta
 7. Great post! Helpful too! As an up and coming blogger myself, I would be honored to be apart of this list.
  Buy real and fake documents

  JibuFuta
 8. utaratutibu ni mzuri ila bado kuna urasimu ktk utengenezaji na upatikanaji wa iyo passpoti kwa maana unaweza kuambiwa wiki mbili passpot tayari ki utaratibu ila inaweza kufika nusu mwaka au zaid apo sasa itategemea na mfuko wako umejaaje..!

  JibuFuta