Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amefanya
ziara ya siku moja katika vituo vya mpakani mkoa wa Kilimanjaro ikiwa na lengo kukagua utendaji kazi wa maafisa na
askari wa Uhamiaji katika vituo hivyo.
Akiwa kituo cha Holili alikagua mpaka na kuongea na watumishi
wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo na kuwasisitiza kufanya kazi kwa weledi na
juhudi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa. Pia aliwataka kuzidisha
doria na ukaguzi maeneo ya mipakani ili kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu.
Katika kituo cha Tarakea, Kamishna Jenerali alikagua mpaka na utendaji kazi katika kituo hicho na baadaye
kuongea na watumishi wa uhamiaji na vyombo vingine vya serikali vinavyofanya kazi katika mpaka huo na kuwataka kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao mpakani hapo.
Pia Kamishna Jenerali alisisitiza watumishi wa uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria za nchi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa, pia aliwataka kuongeza kasi ya kufanya doria maeneo yanayodhaniwa kuwa ni vipenyo vya wahamiaji haramu kuingia nchini.
Pia Kamishna Jenerali alisisitiza watumishi wa uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria za nchi pia kujiepusha na vitendo vya rushwa, pia aliwataka kuongeza kasi ya kufanya doria maeneo yanayodhaniwa kuwa ni vipenyo vya wahamiaji haramu kuingia nchini.
Akiwa katika mpaka wa Rongai, Kamishna Jenerali aliongea na wananchi na kuwataka kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika ulinzi wa mpaka huo na kuwasisisitiza kutoa taarifa za wahamiaji haramu badala ya kukaa kimya na kuangalia tu kwani wananchi waishio mipakani wanalo jukumu kubwa katika ulinzi wa mipaka katika maeneo wanayoishi,
Akiwa mjini Moshi, Kamishna Jenerali
alifungua mafunzo ya Ukaguzi wa nyaraka na kujenga uwezo kwa maafisa wa vyombo ya ulinzi na usalama katika masula ya Ugaidi yaliyoanza
tarehe 8 Februari 2018 katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini
Moshi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akipata maelezo kutoka kwa Mfawidhi wa Kituo cha Uhamiaji katika mpaka wa Tarakea |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisalimiana na Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Uhamiaji Holili wakati wa ziara yake katika kituo hicho |
Msemaji wa Idara Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda akiwa na Afisa Uhusiano wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Mkaguzi wa Uhamiaji Leslie Mbotta |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni