Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

25 Agosti 2018

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji aongoza Watumishi wa Uhamiaji kufanya Usafi Kambi ya Wazee, Walemavu na Wasiojiweza

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makalala, leo siku ya Jumamosi Agosti 25, 2018 ameongoza Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kufanya Usafi katika Kambi ya Wazee, Walemavu na Wasiojiweza iliyopo Nunge Wilayani Kigamboni.

Pamoja na Usafi huo, Kamishna alikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi pamoja na vyakula kwa viongozi wa Kambi ili vitumike kwa ajili ya Wazee, Walemavu na Wasiojiweza katika Kambi hiyo.

#ePassport #eVisa #ePermit #eBorder








24 Agosti 2018

Uzinduzi wa Pasipoti ya Kielektroniki Mkoa wa Pwani katika Picha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo leo tarehe 24 Agosti 2018 amezindua Huduma ya Pasipoti za Kielektroniki katika Mkoa wake mjini Kibaha kwenye Ofisi za Uhamiaji mkoa wa Pwani.

Katika Uzinduzi huo, Mheshimiwa Ndikilo amewaka wananchi wanaopatiwa pasipoti hizo kuzitunza na kuzitumia kwa matumizi sahihi.

"Unakuta mtu yupo humu nchini wala havuki mipaka lakini anatembea na pasipoti, hio si sahihi, tembea na kitambulisho cha Taifa na si pasipoti. Hii ni kwa ajili ya kuvuka mipaka ya nchi na si vinginevyo" alisisitiza Mkuu wa Mkoa.







Afisa Uhamiaji Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Placid Mazengo akiongea na wananchi wakati wa Uzinduzi huo


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Injinia Evarist Ndikilo akiongea na wananchi wa mkoa wa Pwani wakati wa Uzinduzi wa Pasipoti za kielektroniki katika mkoa huo.



Mkuu wa Mkoa Mhe. Ndikilo akimkabidhi pasipoti yake mmoja wa wananchi wa mkoa wa Pwani





13 Agosti 2018

UHAMIAJI YAZINDUA HUDUMA YA PASIPOTI MPYA YA KIELEKTRONIKI JIJINI MWANZA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela amezindua huduma mpya ya Pasipoti za Kielektroniki katika Jiji la Mwanza, hafla iliyofanyika katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoani Mwanza.

Mhe. Mongela amewataka Watanzania kuzitunza pasipoti zao kwa uangalifu na kuzitumia katika njia halali kwavile Pasipoti ni Utambulisho wa Utaifa wa mtu anaposafiri nje ya nchi.
Aidha, Afisa Uhamiaji wa Mkoa Mwanza, Kamishna Msaidizi Paul Eranga alieleza kuwa hadi sasa takribani Mikoa 21 imekwisha fikiwa na huduma tangu kuzinduliwa kwake Januari 23, 2018.

"Tunatarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu, Idara itakuwa imekalimilisha kufunga Mifumo ya utoaji wa Pasipoti hizi Mpya za Kielektroniki kwa nchi nzima. Pia tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Mgufuli azindue Mfumo wa Uhamiaji Mtando hadi sasa Jumla ya Wanzania 30,941 wamepatiwa Pasipoti hizi mpya za Kielektroniki." Aliongeza Naibu Kamishna Eranga.





Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Mhe. John Mongela akisaini kukiri kupokea Pasipoti mpya ya Kielektroniki mbele ya Mwenyeji wake Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Eranga.

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Joseph Mtenga  (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya Maafisa Uhamiaji wa Mwanza wakifuatilia jambo katika hafla ya uzinduzi wa pasipoti mpya ya kielektroniki

Afisa Uhamiaji Mkoa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Eranga akitoa taarifa ya huduma za Uhamiaji katika hafla ya Uzinduzi wa Uhamiaji Mtandao na Pasipoti Mpya za Kielektroniki Jijini Mwanza.


12 Agosti 2018

Uzinduzi wa Pasipoti ya Kielektoniki jijini Mwanza.

Idara ya Uhamiaji inawaalika Watanzania Wote na Wakazi wa jiji la Mwanza kwenye Uzinduzi wa Huduma ya Pasipoti ya Kielekroniki katika Mkoa wa Mwanza. Karibuni.

#ePassport #eVisa #ePermit #eBorder