Kamishna wa Uhamiaji (Uraia na Pasipoti) Kamishna Gerald Kihinga amekabidhi pasipoti mpya za kielektroniki 16 kwa wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa chini ya umri wa miaka 13 (U13) kutoka shule ya Fountain Gate.
Vijana hao wanatarajia kusafiri kwenda nchini Ubelgiji kushiriki mashindano ya Soka ya Dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 13.
Aidha, Kamishna Kihinga aliwapongeza vijana hao kwa kuiwakilisha nchi na kuwataka kucheza kwa juhudi ili walete kombe nchini.
"Leo tumewapatia pasipoti ili muweze kusafiri kwenda kwenye mashindano, pia nawapongeza sana kwa kuchaguliwa kwenu kuiwakilisha nchi yetu, hivyo nawaomba mkacheze kwa juhudi na moyo wa kizalendo ili mchukue kombe na kuiletea sifa nzuri nchi yetu" alisema Kamishna Kihinga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni