Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

20 Agosti 2020

Idara ya Uhamiaji Tanzania yatoa Elimu ya Uraia kwa Tume ya Uchaguzi Vyama vya Siasa na Wadau wa Uchaguzi.

Dar es salaam, Tanzania

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala Mapema wiki hii ametoa elimu ya Uraia katika Mkutano wa Tume ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika Jijini Dar es salaam Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNICC)


Akitoa neno la Utangulizi CGI Dkt. Makakala amesema suala la Uraia ni la kisheria na lina historia ndefu sana kabla ya uhuru, wakati wa Uhuru na bada ya Uhuru.


“Uraia si jambo dogo, ni utambulisho unaokutambua umetoka wapi ? wewe ni nani? Lakini pia uraia ni hadhi na kuwa ni msingi wa uzalendo katika kuitetea na kuipigania nchi” alisema CGI Dkt. Makakala


Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa siasa na watanzania kwa ujumla kuwa na uzalendo kwa kuipenda nchi yao  na kuangalia usalama wa raia wa Tanzania kuwa ndio namba moja ili kuendelea kudumisha Amani na Utulivu uiliopo kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.


Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Uhamiaji Tanzania Mrakibu Paul Mselle akiwasilisha mada ya uraia katika mkutano huo alisema, Uraia ni hali ya mtu kutambulika kuwa na haki na wajibu kwa Taifa la Tanzania.


Raia ni mtu ambaye anatambulika kwa mujibu wa Sheria anapata haki za kiraia ikiwamo kuishi nchini, kupata hifadhi ya kitaifa na kushiriki kwenye masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.


Kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Tanzania Sura ya 357, (Rejeo la mwaka 2002) kuna aina tatu za uraia wa Tanzania ambapo kuna Urai wa kuzaliwa, Uraia wa kurithi , na  Uraia wa Tanzania wa tajnisi


Raia wa Tanzania ana wajibu wa kushiriki katika kuijenga nchi yake na kutii sheria za nchi, pia anawajibu wa kuwa mzalendo kwa Taifa lake kwa kulinda usalama na maslahi ya Taifa kabla ya maslahi yake binafsi.


Masuala ya uraia yanasimamiwa na misingi mikuu miwili ambayo ni uraia unaopatikana kwa njia ya damu (right of blood) na mwingine unaopatikana kwa ardhi alikozaliwa (Jus soli). 


Kihistoria Tanzania tumekuwa tukifuata msingi wa uraia unaopatika kwa njia ya damu, Maana yake uraia wa kuzaliwa unatokana na wazazi wote au mmoja wa wazazi kuwa raia wa Tanzania.


Idara ya Uhamiaji Tanzania ni moja ya chombo cha Ulinzi na Usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo imeanzishwa kwa mujibu kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la mwaka 2016.


Majukumu ya Idara ya Uhamiaji ni Kudhibiti uingiaji, ukaazi na utokaji wa watu nchini, Kutoa huduma za pasipoti na hati nyingine za kusafiria kwa raia, Kutoa hati na vibali vya ukaazi kwa wageni, Kuratibu mchakato wa maombi ya uraia kwa wageni na kumtambua raia kwa mujibu wa sheria.

 HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa Elimu ya Uraia kwa Tume ya Uchaguzi, vyama vya siasa na Wadau wa Uchaguzi wakiwemo Viongozi wa Dini

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Nchini Tanzania Jaji Semistocles Kaijage akiongoza Mkutano wa Tume ya Uchaguzi na Vyama vya Siasa na Wadau wa Uchaguzi

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Mrakibu Paul Mselle Akiwasilisha Mada ya Uraia

Baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa 



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akiendelea kutoa Elimu ya Uraia




Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi akitoa Maelezo ya Kuhusu Sheria na  Gharama na Uchaguzi 2020





Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro akisikliza kwa makini mada zinazotolewa Kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna







Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo Akifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa








Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala akielekea sehemu ya kutolea Elimu ya Uraia katika Ukumbi wa (JNICC)

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Mrakibu Paul Mselle akiendelea kuwasilisha Mada ya Uraia








(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Mkuu)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni