Amesisitiza kuwa Uhamiaji ilikuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za raia watanzania na wageni walioingia na kutoka nchini wakati ule, na hivyo anayo imani kubwa kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa kipindi hiki cha kuelekea uchguzi Mkuu.
Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kutokana na mikakati ya daharura na haraka iliyofanywa na Idara hiyo wakati wa janga la corona, anayo Imani kubwa kwamba Idara ya Uhamiaji itafanya vyema kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2020.
Akitoa taarifa ya Utandaji kazi wa Idara ya Uhamiaji, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala amesema kuwa Idara ya Uhamiaji itahakikisha kuwa inatatua mapingamizi yote ya Uraia dhidi ya Wagombea na kuhakikisha kuwa raia wa Tanzania wanatimiza haki yao ya Kikatiba ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Dkt. Makakala ameongeza kuwa Idara imejipanga vyema na kuhakikisha kuwa raia wa Tanzania wenye sifa ndio watakaoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hata hivyo, Kamishna Jenerali Dkt. Makakala amewataka Wageni wote Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa kufuata sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Uhamiaji ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wakitekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira Akisaini Kitabu cha Wageni |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni