Tarakea, Rombo Kilimanjaro Mkuu wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Mhe. Dkt Athuman Kihamia amefungua Semina ya Siku tatu kuhusu masuala ya kiuhamiaji na uhalifu unaovuka mipaka kwa Viongozi na wananchi wanaoishi maeneo ya mpaka wa Tanzania na Kenya katika kata ya Tarakea. Mhe. Dkt.Kihamia ameishukuru Idara
ya Uhamiaji pamoja na Shirika la Uhamaji la Kimataifa (IOM) kwa kuendesha
Semina ya Masuala ya Kiuhamiaji na Uhalifu unaovuka Mipaka (TransNational
Organized Crime) kwa wakazi wa kata ya Tarakea wakati huu Taifa likielekea kwenye
uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020. “Nimefurahishwa na maamuzi yenu
kuleta Semina hii muhimu ambapo naamini washiriki watajifunza mengi sana kuhusu
Uhamiaji na uhalifu katika maeneo ya mipaka. Elimu mtakayoitoa ni muhimu sana
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Nanyi washiriki niwapongeze kwa
kuchaguliwa kushiriki na kile mtakachokipata basi mkawafikishie jamii
inayotuzunguka ili mpaka wetu na nchi kwa ujumla iwe salama.” Alisema Dk. Kihamia. Semina hii ya siku tatu ya Masuala
ya Kiuhamiaji na Uhalifu unaovuka Mipaka inashirikisha Viongozi wa Serikali,
Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani, Viongozi wa Madhehebu ya Dini,
Viongozi wa Bodaboda, Viongozi wa Wafanyabiashara na wananchi wa Kawaida.
Semina hii
ni muendelezo wa Semina kwa jamii zinazoishi maeneo ya mpakani ikiwa ni mpango
wa Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Wahamaji
Duniani (IOM) kuwashirikisha wananchi kwenye suala zima la ulinzi wa nchi kwa
kushiriki katika udhibiti wa Uhalifu maeneo ya mipakani. |
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Dkt. Athumani Kihamia alipokuwa akiongea wakati wa Ufunguzi wa Semina juu ya Masuala ya Uhamiaji na Uhalifu unaovuka Mipaka (Transnational Crimes), katika mji mdogo wa Tarakea, Mpakani kwa Tanzania na Kenya. |
Afisa Uhamiaji Wilaya Rombo Mrakibu wa Uhamiaji Michael Mtoba akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua semina katika mpaka wa Tarakea, Agosti 18, 2020. |
Mmoja wa Wawezeshaji katika Semina hiyo, Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Aziz Kirondomara akiwasilisha mada ya Dhana ya Uhalifu unaovuka Mipaka na matokeo yake kwa washiriki |
Sehemu ya washiriki wa Semina ya Masuala ya Uhamiaji na uhalifu unaovuka mipaka wafuatilia kwa makini somo linaloendelea |
Muwezeshaji kutoka Shirika la IOM Bi. Lucy Mseke akiwasilisha mada juu ya Dhana ya Biashara ya Binadamu na madhara yake katika semina inayoendelea katika mpaka wa Tarakea. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni