Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

03 Agosti 2020

CGI Dkt. Anna Makakala Ahimiza Nidhamu, Uwajibikaji na Kukataa Rushwa

Mtwara, Tanzania

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala Mapema wiki hiii amefanya ziara ya Kikazi Mkoani Mtwara na kufanya Kikao kazi kilichowakutanisha Maofisa na Askari wa Uhamiaji Mkoani humo, huku akisisitiza suala la Nidhamu Uwajibikaji na kukataa Rushwa.

“Rushwa ni Adui wa haki na sisi tunakauli mbiu yetu nzuri sana inayosema Uhamiaji Upendo, Mshikamano Uwajibikaji na Kukataa Rushwa, na  ni muhimu kutambua kwamba sisi tunatoa huduma na tumepewa dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, ni lazima tusimamie viapo vyetu kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa letu kwa kizazi cha sasa na baadae” alisema  CGI Dkt. Makakala

Kwa upande wake Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Peter Edward Chogero amewakumbusha Maofisa na Askari kuendelea kudumisha Nidhamu ilyopo na kufanya kazi kwa utii, uhodari na weledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya Idara ya Uhamiaji na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewakumbusha Maofisa na Askari kutojihusisha na makundi ya vyama vya  siasa kwani kufanya hivyo ni kinyume na Katiba, taratibu na kanuni kwa Maofisa na Askari waliopo katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama kujihusisha na Makundi hayo au kutangaza nia ya kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa bila kufuata utaratibu unaokubalika.

Akitoa Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mkoa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi (ACI) Novat Dawson amesema Mkoa huo una wahamiaji walowezi ambao wengi wao bado wanaendelea kutambuliwa na kuandikishwa kupitia zoezi la vitambulisho vya Taifa NIDA.

“Mpaka sasa Jumla ya watu 5,524 wametabuliwa na kuandikishwa kama wahamiaji walowezi, pamoja na jitihada za awali tunazoendelea nazo, tunasubiri kuanza kwa zoezi hili rasmi na kuwa na Kanzi Data ya Wahamiaji walowezi, zoezi ambalo linaratibiwa na Idara ya Uhamiaji kwa Kushirikiana na Shirika la Wahamaji Kimataifa IOM” Alisema ACI Dawson

Mkoa wa Mtwara una wilaya 05 na zote zinapakana na nchi jirani ya Msumbiji Mpaka wa Asili ukiwa ni mto Ruvuma, Kuna vituo 03 vya kutoa huduma za Kiuhamiaji katika Mpaka wa bonde la Mto Ruvuma ambavyo ni (Kilambo, Mkunya, na Mtambaswala), Aidha kunavituo viwili ambavyo ni Bandari na Uwanja wa Ndege ambavyo huduma zake husimamiwa na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwasili Katika Ofisi yaUhamiaji Mkoa wa Mtwara
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akisisitiza Jambo
Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Peter Edward Chogero akiongea na Maofisa na Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara (hawapo Pichani)Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi (ACI) Novat Dawson akitoa Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mkoa 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya pamoja na Maofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiwa katika Picha ya pamoja na Askari (NCO) Uhamiaji Mkoa wa Mtwara (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni