Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

06 Agosti 2020

Ziara ya CGI Dkt. Anna Makakala Mkoani Lindi yafana sana

Lindi, Tanzania


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala aliendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Lindi  ambapo alitembelea eneo la Ujenzi wa Ofisi mpya ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi na baadae kufanya kikao kazikwa kuongea na Maofisa na Askari wa Uhamiaji Mkoani hapo.

CGI Dkt. Makakala alisisitiza suala zima la Nidhamu Utii, Uaminifu  na kufanya kazi kwa Uhodari na weledi wa hali ya juu ili kuilinda na kuitetea nchi yetu kwa faida ya sasa na baadae.

Aidha ameendelea kukemea vitendo vya rushwa na kuwataka maafisa na askari wote wa uhamiaji kutojihusisha kabisa na Rushwa bali waendelee kutoa huduma bora  zenye viwango vya Kimataifa    kwa wananchi na wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Katika Maelekezo yake pia ameutaka Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa Ujumla kuendelea kufanya doria na misako ya mara kwa mara ili kupunguza na kukomesha kabisa suala la Wahamiaji haramu.

Katika Kutekeleza majukumu yake na kutoa huduma bora kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wageni Idara ya Uhamiaji inaendelea kufanya mabadiliko na maboresho ya mifumo mbalimbali ya utoaji huduma kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Uhamiaji Kielekroniki) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma husika.

Mifumo hiyo ni pamoja na huduma za kielekroniki za utoaji wa Pasipoti, Visa, Vibali vya Ukaazi na Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka.

Katika ziara hiyo CGI Dkt. Anna Makakala aliambatana na Kamishna wa Utawala na Fedha (CI) Edward Peter Chogero, ambae aliwataka Maofisa na Askari kuendelea kufanya kazi kwa kufuata Taratibu, Kanuni na miongozo inayotolewa ili kutimiza wajibu wao sanjari na kudumisha nidhamu na uwajibikaji kwa maendeleo ya Taifa letu.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala


Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Edward Chogero akiongea na Maofisa na Askari waa Uhamiaji Mkoa wa Lindi kulia nia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala 
Ujenzi Unaaendelea Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi

Baadhi ya Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi wakimsikiliza kwa Makini CGI Dkt. Anna Makakala
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji  (ACI) Marco Mumwi
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Nafro Mageta akitoa Ripoti ya Maofisa na Askari kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala (Hayupo Pichani) Wakati wa Ziara yake ya Kikazi hivi karibuniJengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi Likiwa katika Hatua ya Ujenzi (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni