NAMNA YA KUJAZA FOMU ZA
MAOMBI YA PASIPOTI
KWA NJIA YA MTANDAO.
2. NENDA KATIKA KITUFE
KILICHOANDIKWA
e - Services. (https://www.immigration.go.tz/ppt_application/)
3. NENDA KWENYE PASSPORT APPLICATION FORM (BOFYA).
4. (i)KWA
MTU AMBAYE ANAJAZA FOMU KWA MARA YA KWANZA KWA NJIA YA MTANDAO ANATAKIWA
KUBOFYA NAMBA 1. OMBI JIPYA.
(ii) KWA AMBAYE
ALIKWISHAJAZA FOMU MTANDAONI HAPO KABLA, NA KUPEWA NAMBA YA OMBI HUSIKA,
ATACHAGUA OMBI LINALOENDELEA ATAINGIZA NAMBA YAKE YA OMBI NA JINA LAKE LA
UKOO.
5. KWA
MTU ANAYEJAZA KWA MARA YA KWANZA ATALETEWA MWONGOZO WENYE MAELEZO YA SIFA ZA
MWOMBAJI. BAADA YA KUSOMA MAELEZO YA UKURASA HUU. BOFYA KITUFE CHA KUKUBALIANA NA MAELEZO YALIYOPO KWENYE UKURASA HUU NA
KISHA UTAENDELEA.
6. BAADA
YA KUKAMILISHA HATUA YA TANO, MWOMBAJI ATAPELEKWA KATIKA UKURASA WA ONLINE PASSPORT APPLICATION NA HAPO ATATAKIWA
KUJAZA KILA KIPENGELE KUANZIA SEHEMU YA TAARIFA
BINFSI.
7. UNAPOJAZA
ZINGATIA KUFUATA MAELEKEZO YA NAMNA YA UJAZAJI (FORMAT) YALIYO AINISHWA KWENYE UKURASA HUSIKA.
8. BAADA
YA KUKAMILISHA BOFYA KITUFE - KUPAKUA
FOMU.
9. ITAKULETEA
FOMU YAKO YA MAOMBI ULIYOJAZA NA HATI YA DHAMANA. UTAHAKIKI TAARIFA ZAKO NA
KISHA KUICHAPA (PRINT) FOMU HIYO PAMOJA NA HATI YA DHAMANA HUSIKA.
10. HATI YA DHAMANA INATAKIWA
IJAZWE NA WATU WATANO (05) TOFAUTI, YAANI WADHAMINI WAWILI (02) NA MASHAHIDI
WATATU (03).
NB:
FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI INAWEZA KUJAZWA MAHALI POPOTE
PENYE HUDUMA YA INTERNET, AMBAPO MWOMBAJI ALIPO, NA WALA MWOMBAJI HALAZIMIKI
KWENDA KUJAZIA FOMU HIYO JIRANI NA OFISI ZA UHAMIAJI.
Imetolewa na Kitengo cha Mahusiano-Uhamiaji Makao Makuu
Namna ya kujaza Fomu Mtandaoni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni