Uhamiaji Mtandao (e-immigration) ni muunganiko
wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa
taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji.
Kupitia teknolojia hiyo, Idara itaweza kutoa;
Kupitia teknolojia hiyo, Idara itaweza kutoa;
·
Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki (e-
Residence Permit),
·
Pasipoti za Kielektroniki (e-Passport)
·
Pamoja na kusimamia masuala ya mipaka
kielektroniki (e-Border Management).
· Viza za kielektroniki (e-Visa)
Mfumo huo wa Uhamiaji Mtandao unalenga kutusaidia;
· Viza za kielektroniki (e-Visa)
Mfumo huo wa Uhamiaji Mtandao unalenga kutusaidia;
· kutoa Pasipoti ya
Kielektroniki ya Afrika Mashariki (e-Passport) ambayo imetengenezwa kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ambapo itakuwa na ‘chip’ iliyobeba
taarifa mbalimbali za mwombaji pamoja na alama nyingi za kiusalama “Security
Features”
· Mfumo utasaidia
kudhibiti na kuwezesha Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Raia na Wageni wanaoingia
nchini kwa madhumuni mbalimbali hususan katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja
na kutunza kumbukumbu zao. Hii itasaidia kuzuia ongezeko la wahamiaji haramu
nchini.
· Pia utasaidia usimamizi
wa utoaji viza na mwombaji atawasilisha maombi yake kwa njia ya kielektroniki;
hii itasaidia kupata taarifa za malipo ya viza kwa wakati na, kudhibiti upotevu
wa maduhuli ya Serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni