Idara ya Uhamiaji imekabidhiwa nyumba 63 ambazo zilizinduliwa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Magufuli
mwishoni mwa mwaka jana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Nyumba hizo ambazo zipo katika
eneo la Iyumbu Manispaa ya Dodoma zilipokelewa na Kamishna Uhamiaji (Utawala na
Fedha) Peter Chogero kutoka kwa Maafisa wa Shirika la Nyumba jana Jumatano 25 Januari 2018.
"Nashukuru sana
kukabidhiwa hizi nyumba kwa kuwa sasa maafisa wataweza kuhamia mara moja. Idara
inatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais kwa kutupatia nyumba hizi"
Alisema Kamishna Chogero.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni