Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

15 Februari 2023

KATIBU MKUU MMUYA AISHUKURU IOM KWA UJENZI WA OFISI MPYA ZA UHAMIAJI (W) MKOANI MTWARA.

Na. Amani Mbwaga, Tandahimba - Mtwara.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya amelishukuru na kulipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji (IOM)Tanzania kwa kulijengea Jeshi la Uhamiaji Ofisi za Uhamiaji Wilaya Mkoani Mtwara.

Bw. Mmuya ameonesha kuridhishwa kwake na ubora wa Majengo hayo ya Ofisi Mpya 04 za Uhamiaji Wilaya ikiwemo Wilaya ya Nanyumbu, Wilaya ya Masasi, Wilaya ya Newala na Wilaya ya Tandahimba huku Ukarabati wa Ofisi ya Uhamiaji Kilambo ukifanyika.

Katibu Mkuu Mmuya ameyasema hayo jana tarehe 14 Februari 2023 Wilayani Tandahimba Mkani Mtwara wakati akihitimisha  ziara yake ya kikazi ya siku 02 ya  kukagua miradi ya ujenzi ya ofisi mpya za Uhamiaji Wilaya zinazojengwa Mkoani Mtwara kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji (IOM) chini ya mradi wao wa "Strengthening Community Engagement and Policing (CEP) and Integrated Border Management (IBM) in Cabo Delgado, Mozambiq and Mtwara United Republic of Tanzania" uliofadhiliwa na serikali ya Shirikisho la Ujerumani kupitia ofisi yake ya Mambo ya Nje.

Malengo ya mradi huo ilikuwa ni kuihusisha jamii za maeneo ya mipakani  kusaidia kulinda mipaka, kuwajengea uwezo Maafisa na Askari kwa kuwapa mafunzo ya usalama wa mipaka, kufanya ununuzi wa vifaa na vitendea kazi katika Mkoa wa Twara na Kufanya mikutano ya ujirani mwema na upande wa Msumbiji  kwa lengo la kuimarisha usalama wa maeneo ya mpakani.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mrakibu wa Uhamiaji Lenatus Mwambene ambae pia ndie Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia Uhamiaji Tanzania alisema Jeshi la Uhamiaji lilifanya tathimini ya ununuzi wa vifaa kama kipengele mojawapo cha utekelezaji wa mradi ambacho kilitengewa fedha kiasi cha Euro 400,000/= kutokana na tathimini iliyofanyika.

Jeshi la Uhamiaji lilishauri na kupendekeza fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa zitumike pia kufanya ujenzi wa ofisi ya kutunza vifaa ambavyo vingenunuliwa na mazingira bora ya kufanyian kazi kwa maafisa na askari.

IOM waliridhia ombi na ushauri huo na ndipo taratibu za kufanikisha ujenzi wa ofisi hizo ulipoanza, aidha ununuzi wa vifaa vya ofisi  tayari vilishanunuliwa na IOM na kukabidhiwa.

Makabidhiano ya eneo la mradi wa ujenzi wa ofisi hizo yalifanyika kuanzia tarehe 03-06 Agosti 2022 kwa kuwakabidhi wakandarasi  maeneo yote  kwa siku nne (04), zoezi hilo lilijumuisha maafisa kutoka IOM, Uhamiaji Pamoja na wakandarasi na ilitarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi mitano (05) kuanzia tarehe 02 Januari 2023 kwa ofisi za Tandahimba na Newala na tarehe 25 Januari 2023 kwa ofisi za Masasi, Nanyumbu na Kilambo lakini tarehe za ukamilishaji wa mradi  uliongezwa kwa kila mkandarasi  kwa muda wa mwezi mmoja na mpaka sasa miradi yote imekamilika kwa zaidi ya asilimia 97% na mara itakapokamilika rasmi Mkandarasi atamkabidhi IOM  na IOM Itakabidhi miradi hiyo kwa Jeshi la Uhamiaji tayari kwa matumizi ya kuwahudumia rai ana wageni kutoka Nchio mbalimbali.

Akihitimisha taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo Mrakibu Mwambene alisema mradi huo ukikamilika utwezesha Jeshi la Uhamiaji kuepukana na gharama kubwa za upangaji katika majengo ya watu binafsi pia itaimarisha ulinzi na usalama sanjari na kuleta ufanisi zaidi katika utendaji kazi kwa maafisa na askari.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mkuu wa Wilaya Nanyumbu ambae pia anakaimu Wilaya ya Tandahimba Mhe. Mariam Chaurembo ameishukuru IOM kwa ufadhili huo na kuahidi Mkoa mzima na Wilaya zake zitashirikiana kuahakikisha zinatunza miradi hiyo kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti, amesema shirika hilo liteendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ki-Uhamiaji ili kuhakikisha kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.

Aidha Bw. Busatti ameongeza kwamba Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji katika kutekeleza mambo mbalimbali ya Ki-uhamiaji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Nae Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji ambae pia ndie Kamishna wa Fedha na Utawala Uhamiaji Makao Makuu Kamishna Hamza Shabani ameipongeza IOM na kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendeleza mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali sanjari na mashirika yake ya Umoja wa Mataifa hali inayopelekea kuchochea maendeleo chanya ya Taifa letu.


HABARI PICHA NA MATUKIO

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nanyumbu wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni ya kukagua miradi ya ujenzi wa ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania.



Muonekano wa Jengo Jipya la Uhamiaji (W) Nanyumbu Mkoani Mtwara




Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia Uhamiaji Tanzania Mrakibu Lenatus Mwambene ambae pia ndie Mratibu wa Ujenzi wa Ofisi hizo akitoa taarifa ya ujenzi kwa Katibu Mkuu Bw. Kaspar Mmuya (Hayupo Pichani) 



Muonekano wa Pembeni wa Ofisi Mpya ya Uhamiaji Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara

Mkandarasi akisoma taarifa yake ya ujenzi kwa Katibu Mkuu Bw. Kaspar Mmuya (hayupo pichani)





Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya kushoto akitoa maelekezo kwa Mkandarasi na watendaji wa Uhamiaji  wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi pya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama (W) Nanyumbu, Mkandarasi Maofisa na Askari  wa Uhamiji wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania kushoto kwake ni Mkuu wa IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti



Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti  na Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia Uhamiaji Tanzania Mrakibu Lenatus Mwambene ambae pia ndie Mratibu wa Ujenzi wa Ofisi hizo wakipongezana kwa kazi nzuri


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Masasi wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania.




Muonekano wa Ofisi Mpya ya Uhamiaji Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara

Muonekano wa Ofisi ya zamani ya Uhamiaji Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara





Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo Jipya la Uhamiaji Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama (W) Masasi, Mkandarasi na Maofisa na Askari  wa Uhamiji wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania kushoto kwake ni Mkuu wa IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkaguzi wa Uhamiaji Frank Mtauka ambae ndie Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Kilambo Mkoani Mtwara alipofika kituoni hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa Kituo cha Uhamiaji Kilambo








Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akipata maelezo ya ukarabati wa jengo la Uhamiaji Kilambo kutoka kwa Mfawidhi wa Kituo hicho Mkaguzi Frank Mtauka.






Muonekano wa Kituo cha Uhamiaji Kilambo Mkoani Mtwara mara baada ya kufanyiwa Ukarabati na IOM Tanzania




Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Newala alipofika kwa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya Newala iliyofadhiliwa na IOM 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Newala

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Newala Mkoani Mtwara


Muonekeno wa Jengo Jipya la Ofisi ya Uhamiaji (W) Newala Mkoani Mtwara lililojengwa kwa ufadhili IOM




Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Maafisa na Askari wa Uhamiaji Wilaya ya Newala Mkoni Mtwara



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akiangalia ramani ya ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji Newala Mkoani Mtwara.



Muonekano wa Pembeni wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara


Ukaguzi Ukiendelea Ofisi ya Uhamiaji Newala



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama (W) Newala, na Maofisa na Askari  wa Uhamiaji wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania Kushoto kwake ni Mkuu wa IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti


Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti (Kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Kaspar Mmuya wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji Wilaya Newala Mkoani Mtwara

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ambae pia ndie Mkuu wa Wilaya Nanyumbu Mhe. Mariam Chaurembo


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Mwakilishi wa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Tandahimba Konstebo Ally Lema wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa ofisi mpya ya Uhamiaji (W) Tandahimba Mkoani Mtwara uliofadhiliwa na IOM


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara


Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti (Kushoto) akisalimiana na Mhe. Mariam Chaurembo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya akipewa zawadi ya korosho kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ambae pia ndie Mkuu wa Wilaya Nanyumbu Mhe. Mariam Chaurembo


Muonekano wa Jengo Jipya la Uhamiaji Wilaya ya Tandahimba lililojengwa kwa Ufadhili wa IOM Tanzania





Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Mariam Chaurembo akiishukuru serikali na Shirika la Kimataifa la Wahamaji IOM Kwa kukamilisha ujenzi wa Ofisi hiyo Wilayani Tandahimba

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kaspar Mmuya (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama (W) Tandahimba, na Maofisa na Askari  wa Uhamiaji wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika kukagua miradi ya ujenzi wa Ofisi mpya za Uhamiaji (W) zinazojengwa Mkoani Mtwara chini ya Ufadhili wa IOM Tanzania Kulia kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya ni Mkuu wa IOM Tanzania Bw. Maurizio Busatti




Baadhi ya Askari wa Uhamiaji Wilayani Tandahimba wakiwa katika picha ya pamoja kwenye jengo lao jipya lilifadhiliwa na IOM Tanzania

(Picha zote na Amani Mbwaga kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Uhamiaji Makao Makuu)