Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala mnamo siku ya Jumatatu Februari 8, 2020 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja jijini Dar es salaam. Katika ziara hiyo, Dkt. Makakala amemtembelea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge na kuongea nae kuhusu masuala ya uhamiaji katika mkoa huo.
Kamishna Jenerali pia alitembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya
ya Ubungo na kuongea na Mkuu wa Wilaya Mh. Kisare Makori, ambapo pia alifanya
ukaguzi wa ofisi ya Uhamiaji (W) Ubungo na kuzungumza na Askari pamoja na Watumishi
kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili. Baada ya mazungumzo hayo,
Kamishna Jenerali alikwenda kukagua kituo kipya cha Uhamiaji ndani ya stendi
mpya ya Mabasi Ubungo.
Ziara hiyo ya Siku moja jijini Dar es salaam ilifikia
tamati kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kukagua kiwanda cha uchapishaji na ushonaji
cha Idara ya uhamiaji kilichopo kijichi Jijini Dar es salaam. Katika ukaguzi
huu alisisitiza watendaji waongeze kasi na weledi ili kufikia malengo yanayotarajiwa.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisikiliza maelezo ya namna ya shughuli za ushonaji zinavyofanyika katika Kiwanda cha Ushonaji cha Uhamiaji, Kijichi Dar es salaam |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Abubakar Kunenge mara baada ya mazungumzo ya kikazi katika ofisi za mkuu huyo wa mkoa. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni