Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Januari 2018

Hii ndio Pasipoti Mpya ya Tanzania ya Kielektroniki iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais






Fahamu kuhusu Uhamiaji Mtandao

Uhamiaji Mtandao (e-immigration) ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja na kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji.

Kupitia teknolojia hiyo, Idara itaweza kutoa;
·           Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki (e- Residence Permit),
·           Pasipoti za Kielektroniki (e-Passport)
·           Pamoja na kusimamia masuala ya mipaka kielektroniki (e-Border Management).
·           Viza za kielektroniki (e-Visa)

Mfumo huo wa Uhamiaji Mtandao unalenga kutusaidia;
·         kutoa Pasipoti ya Kielektroniki ya Afrika Mashariki (e-Passport) ambayo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo itakuwa na chip’ iliyobeba taarifa mbalimbali za mwombaji pamoja na alama  nyingi za kiusalama “Security Features”
·         Mfumo utasaidia kudhibiti na kuwezesha Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Raia na Wageni wanaoingia nchini kwa madhumuni mbalimbali hususan katika maeneo ya mipakani ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu zao. Hii itasaidia kuzuia ongezeko la wahamiaji haramu nchini.

·         Pia utasaidia usimamizi wa utoaji viza na mwombaji atawasilisha maombi yake kwa njia ya kielektroniki; hii itasaidia kupata taarifa za malipo ya viza kwa wakati na, kudhibiti upotevu wa maduhuli ya Serikali.

26 Januari 2018

Mkutano wa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Uhamiaji

Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi jana tarehe 25 Januari 2018 alifanya mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu.

Katika mkutano huo, alitoa maagizo mbalimbali na pia kusimamisha utoaji wa pasipoti kwa vijana wanaokwenda nje ya nchi kufanya kazi za ndani na nyinginezo ambapo imeripotiwa kuwa pindi wakiwa huko ughaibuni huteswa, kunyanyaswa na hata kuuwawa.






25 Januari 2018

UHAMIAJI YAKABIDHIWA RASMI NYUMBA ZA IYUMBU DODOMA

Idara ya Uhamiaji imekabidhiwa nyumba 63 ambazo zilizinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Magufuli mwishoni mwa mwaka jana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Nyumba hizo ambazo zipo katika eneo la Iyumbu Manispaa ya Dodoma zilipokelewa na Kamishna Uhamiaji (Utawala na Fedha) Peter Chogero kutoka kwa Maafisa wa Shirika la Nyumba jana Jumatano 25 Januari 2018.

"Nashukuru sana kukabidhiwa hizi nyumba kwa kuwa sasa maafisa wataweza kuhamia mara moja. Idara inatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais kwa kutupatia nyumba hizi" Alisema Kamishna Chogero.










21 Januari 2018

Huduma halali za Pasipoti, Epuka Upotoshwaji.

       Pasipoti hutolewa kwa Raia wa Tanzania tu.
       Na ni haki ya kila Mtanzania, Timiza wajibu wako.
       Zingatia Taratibu za Uombaji na Utoaji wa Pasipoti.

Maombi ya Pasipoti huwasilishwa na mwombaji mwenyewe katika Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, Afisi ya Uhamiaji Zanzibar, au kwenye ofisi yoyote ya Uhamiaji Mkoa ama Wilaya anayoishi mwombaji au Ofisi za Balozi za Tanzania kwa waombaji wanaoishi nchi za nje.

Huduma zote za Uhamiaji hazina Uwakala – Epuka Mawakala/Vishoka


17 Januari 2018

NAMNA YA KUJAZA FOMU MTANDAONI


NAMNA YA KUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA PASIPOTI 
KWA NJIA YA MTANDAO.

1.  INGIA KATIKA TOVUTI

https://www.immigration.go.tz/

2.  NENDA KATIKA KITUFE KILICHOANDIKWA 



3. NENDA KWENYE PASSPORT APPLICATION FORM (BOFYA).

4.  (i)KWA MTU AMBAYE ANAJAZA FOMU KWA MARA YA KWANZA KWA NJIA YA MTANDAO ANATAKIWA KUBOFYA NAMBA 1. OMBI JIPYA.

(ii)  KWA AMBAYE ALIKWISHAJAZA FOMU MTANDAONI HAPO KABLA, NA KUPEWA NAMBA YA OMBI HUSIKA, ATACHAGUA OMBI LINALOENDELEA ATAINGIZA NAMBA YAKE YA OMBI NA JINA LAKE LA UKOO.

5. KWA MTU ANAYEJAZA KWA MARA YA KWANZA ATALETEWA MWONGOZO WENYE MAELEZO YA SIFA ZA MWOMBAJI. BAADA YA KUSOMA MAELEZO YA UKURASA HUU. BOFYA KITUFE CHA KUKUBALIANA NA MAELEZO YALIYOPO KWENYE UKURASA HUU NA KISHA UTAENDELEA.

6. BAADA YA KUKAMILISHA HATUA YA TANO, MWOMBAJI ATAPELEKWA KATIKA UKURASA WA ONLINE PASSPORT APPLICATION NA HAPO ATATAKIWA KUJAZA KILA KIPENGELE KUANZIA SEHEMU YA TAARIFA BINFSI.

7.  UNAPOJAZA ZINGATIA KUFUATA MAELEKEZO YA NAMNA YA UJAZAJI (FORMAT) YALIYO AINISHWA KWENYE UKURASA HUSIKA.

8.  BAADA YA KUKAMILISHA BOFYA KITUFE - KUPAKUA FOMU.

9.  ITAKULETEA FOMU YAKO YA MAOMBI ULIYOJAZA NA HATI YA DHAMANA. UTAHAKIKI TAARIFA ZAKO NA KISHA KUICHAPA (PRINT) FOMU HIYO PAMOJA NA HATI YA DHAMANA HUSIKA.

10.    HATI YA DHAMANA INATAKIWA IJAZWE NA WATU WATANO (05) TOFAUTI, YAANI WADHAMINI WAWILI (02) NA MASHAHIDI WATATU (03).

NB:
FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI INAWEZA KUJAZWA MAHALI POPOTE PENYE HUDUMA YA INTERNET, AMBAPO MWOMBAJI ALIPO, NA WALA MWOMBAJI HALAZIMIKI KWENDA KUJAZIA FOMU HIYO JIRANI NA OFISI ZA UHAMIAJI.


Imetolewa na Kitengo cha Mahusiano-Uhamiaji Makao Makuu

Uhamiaji Rwanda walivyoshiriki Sikukuu za Krismass na Mwaka Mpya 2018 na Uhamiaji Tanzania.


Ukaguzi wa Wageni nchini Mkoa wa Kagera


Sheria Ya Uhamiaji Sura 54 Rejeo la 2016 inampa mamlaka Afisa Uhamiaji kumsimamisha mtu yeyote na kumhoji juu ya Uhalali wake wa kuwepo nchini Tanzania. Hapa ni Afisa Uhamiaji kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera Sajini Elia Mlay akimkagua raia wa Poland kujiridhisha uhalali wake wa kuishi nchini.