Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

30 Novemba 2017

Watumishi wa Kada ya Kiraia wa Uhamiaji wafanya Mkutano wa kutathmini utendaji kazi wa Idara kwa mwaka 2017

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Maj. Gen. Projest Rwegasira aliwaasa Watumishi wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na nidhamu.

Akizungumza na Watumishi hao kwenye Mkutano huo uliofanyika jana TRITA Moshi Katibu Mkuu aliongeza kuwa Viongozi wa Idara ya Uhamiaji na Watumishi wengine watumie Mkutano huo kutathmini mafanikio na changamoto mbalimbali zinazokwamisha utendaji kazi wa Idara.

"Natambua kuwa vikao vya aina hii vipo kwa mujibu wa Sheria, lakini pia ni muhimu sana kwa watumishi wa Kada ya kiraia ambao wanafanya kazi katika Vyombo ambavyo mfumo wake wa uendeshaji ni wa kijeshi zaidi wakapata fursa ya kusikilizwa hoja zao, kwani ipo dhana miongoni mwa watumishi raia kuwa hawapati fursa ya kushiriki na kufahamu baadhi ya mambo muhimu yanayohusu maslahi yao katika Vyombo hivyo. Mimi naamini Baraza hili ni uwanja mzuri sana na uliowazi katika kujadili masuala mbalimbali yanayo gusa maslahi ya mtumishi pamoja na mwajiri wake mahala Pa Kazi. Hivyo muutumie vizuri uwanja huu kwa maslahi ya pande zote mbili" alisema Katibu Mkuu.

Hili ni Baraza kubwa la Kitaifa la Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Tanzania TUGHE ambalo hufanyika kila mwaka likiwa na lengo la kutathmini utendaji kazi na kushughulikia maslahi ya Watumishi wa Kada ya Kiraia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (Mwenyekiti), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar (Makamu Mwenyekiti), Makamishna wa Uhamiaji wa Divisheni za Fedha na Utawala, Pasipoti na Uraia, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Viza na Pasi, Vibali vya Ukaazi na Wafawidhi wa Vitengo toka Uhamiaji Makao Makuu na Zanzibar.

Kadhalika Viongozi wa TUGHE tawi la Uhamiaji Bw. Shaame A. Hamad (Mwenyekiti), Triphonia J. Kimaro (Katibu), Eng. Amani Msuya (Naibu Katibu TUGHE - Taifa), Bi. Magreth Ngomuo (Katibu Baraza) na Naibu Katibu Baraza Bw. Tale Ndonje ni miongoni mwa viongozi  ambao walifanikisha na kuhudhuria Mkutano huo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Maj. Gen. Projest Rwegasira akiwasili katika Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA).

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar akiwasili katika Chuo cha Uhamiaji Cha Kikanda (TRITA) kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiwaongoza Makamishna wengine kumpokea Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya NchiMwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna P. Makakala akimuongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Maj. Gen. Projest Rwegasira kuingia kwenye ukumbi wa mkutanoWajumbe wakiwasili kwenye ukumbi wa mkutano
Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji TRITA Commandant Maurice Kitinusa akiwakaribisha wajumbeViongozi wa Baraza wakiwaongoza wajumbe kuimba wimbo wa Watumishi 'Solidarity forever'


24 Novemba 2017

ZIARA YA KAMISHNA WA UHAMIAJI VIZA NA PASI KATIKA MIKOA YA DODOMA, IRINGA NA NJOMBE KATIKA PICHA


Kamishna wa Uhamiaji Viza na Pasi, Mwichum  Salum  amefanya ziara katika Mikoa ya Dodoma,Iringa na Njombe kuongea na Maafisa na askari wa Uhamiaji kupanga mikakati ili kuzidisha utendaji wa kazi wa idara,aidha Kamishna Mwichum ametembela vituo vya wilayani kujionea hali halisi ya utendaji kazi. 
Kamishna wa Uhamaiji Viza na Pasi Mwichum H Salum  akisikiliza taarifa ya utendaji kazi  kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Naibu Kamishna wa Uhamiaji Peter Jerome Kundy

Kaimishna wa Uhamiaji Viza na Pasi Mwichum Salum akimsikiliza Afisa uhamiaji mkoa wa Njombe  Kamishna msaidizi Hosseh Kagimbo kwenye kituo cha Makambako

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Naibu Kamishna wa Uhamiaji Peter Jerome Kundy akisoma taarifa ya utendaji kazi kwenye kikao pamoja na wafanyakazi wa mkoa wa Dodoma.
Kamishna wa Uhamiaji Viza na Pasi Mwichum  Salum wa pili kutoka kushoto akiwa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Njombe  Kamishna Msaidizi  Hosseh Kagimbo wa kwanza kutoka kushoto na msaidizi wake pamoja na Maafisa wa kituo cha Makambako
Maafisa wa Uhamiaji Mkoa wa Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Uhamiaji Viza na Pasi baada ya kikao alichokifanya wakati wa ziara yake Mkoani hapo.
Kamishna wa Uhamiaji Viza na Pasi Mwichum Salum akiwa katika picha ya pamoja na maafisa na askari wa Mkoa wa Dodoma baada ya kikao.

Kamishna wa Uhamiaji Visa na Pasi Mwichum Saluh akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Njombe kwenye eneo ambalo ofisi ya Uhamiaji Mkoa 
itajengwa hapo baada ya Halmashauri kutenga maeneo ambayo ofisi zote za umma zitajengwa eneno hilo. 
JE UNAHITAJI PASIPOTI?


23 Novemba 2017

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KUSINI UNGUJA

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utaratibu wa kawaida kutembelea vituo na ofisi za uhamiaji Zanzibar.

Ziara hiyo iliyokuwa na malengo makuu mawili, Kwanza ni kukagua miradi mbalimbali na viwanja vilivyopo katika Mkoa huo. Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi Watumishi na ofisi ni hatua muhimu katika kutanua wigo wa utoaji huduma mbali mbali za Uhamiaji kwa Wilaya zote za Unguja na Pemba ambayo ni utekelezaji wa ahadi za Serikali kuwafikishia wananchi wake huduma katika maeneo wanayoishi.

Pili, ilikuwa ni kuhimiza askari na maafisa uhamiaji kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na kujituma ili wananchi wapate huduma kwa wakati.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Khamis Ali Juma kutoka katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja alimweleza Kamishna maendeleo ya miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi na ofisi katika mkoa huo pamoja na namna walivyojipanga kutoa huduma kwa weledi.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu, alieleza jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika ujenzi wa Makazi ya Askari wake katika Wilaya zote Unguja na Pemba.

"Nimekuja kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Watumishi hapa Makunduchi, Wilaya ya Kusini. Ujenzi unaendelea vizuri, tunategemea zikikamilika zitapunguza tatizo la upungufu wa nyumba za makazi ya watumishi. Tunavyo viwanja katika mkoa huu, tunategemea kununua viwanja vingine kwa ajili ya miradi hapo baadae.” Alieleza Kamishna wa Uhamiaji huyo.

Ziara hiyo ya siku mbili katika Mkoa wa Kusini Unguja imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwani kero mbalimbali zilipatiwa majibu ya kuridhisha pamoja na miradi iliyokaguliwa kubainika kuwa inakwenda vizuri. Kamishna Uhamiaji wa Zanzibar pamoja na majukumu mengine amekuwa akitembelea Ofisi na Vituo vya Uhamiaji Unguja na Pemba kuhimiza utendaji kazi unaofuta misingi na sheria. 


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu akisisitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini wakati ya ziara yake katika mkoa huo.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa nyumba za makazi ya watumishi zinazohitaji ukarabati.


Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Khamis Ali Juma kutoka katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja akimweleza Kamishna wa Uhamiaji juu ya maendeleo ya miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi na ofisi katika mkoa huo.


Maafisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakiambatana na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (katikati), wakati alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Kati na Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Hapa ilikuwa ni ukaguzi Viwanja vilivyopo Mkoani wa Kusini Unguja.


22 Novemba 2017

WALIOKWENDA CHINA WAREJEA SALAMA NCHINI

Maafisa Uhamiaji 15 waliokwenda nchini China kwenye ziara ya mafunzo ya wiki mbili wamerejea nchini jana usiku wakitokea katika jiji la ShangChuan ambapo walipokelewa na Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Ignasio Gunda Mgana.


Msafara huo ulifika Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar leo majira ya saa tatu asubuhi na kulakiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga ambaye alipokea taarifa ya safari na mafunzo.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo alieleza namna walivyosafiri na kupokelewa na uongozi wa chuo cha Uhamiaji jimbo la ShangChuan na mafunzo waliyopata.

“Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu kutuwezesha kwenda na kurudi salama, Afande naomba ufahamu kuwa wale wenzetu wa China walitupokea na kutukirimu sana. Mafunzo tuliyopata ndani ya wiki mbili hizo ni masuala ya Human trafficking, border management issues, smuggling, cybercrime, customer care na travel documents verification. Kwa kweli tumejifunza mambo mengi ambayo yametufungua na yatatusaidia sana katika utendaji kazi wetu wa kila siku, asante afande kwa kutuchagua kuiwakilisha idara katika mafunzo haya’’ alieleza Mwanzalima.

Naye Kaimu Kamishna wa Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga aliwataka maafisa hao kutumia ujuzi waliopata katika mafunzo hayo ili kuboresha huduma za uhamiaji  na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi wanaofika kwenye ofisi za uhamiaji.Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima akimweleza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga juu ya safari yao ya China na Mafunzo waliyopata.


Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Ignas Gunda Mgana (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya safari ya maafisa walikwenda nchini kwenye mafunzo ya wiki mbili

Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima akitoa taarifa ya safari ya mafunzo nchini China

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji Hannelore Manyanga akipokea zawadi ya Ngao ya Urafiki na Ushirikiano baina ya  Tanzania na Idara ya Uhamiaji na Polisi ya China


Picha ya pamoja wa maafisa walio rejea kutoka nchini China na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (aliyekaa).