Jumla ya Maafisa Uhamiaji 15 wameagwa leo jijini Dar es
salaam tayari kwa safari kuelekea nchini China kwa ajili ya mafunzo ya wiki
mbili.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini wilaya ya
Temeke iliwakutanisha maafisa uhamiaji kutoa maeneo mbalimbali nchini ambao
wanasafiri mwisho wa wiki hii.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga
aliwatakia safari njema maafisa hao na kuwasisitiza kuzingatia mafunzo
watakayopewa ili waje kutumia ujuzi watakaoupata kwa ajili ya maendeleo ya
Idara.
Maafisa hao wanategemea kuondoka nchini mwishoni mwa wiki
kuelekea jijini ShangChuan.
Maafisa Uhamiaji wanaosafiri mwishoni mwa wiki kuelekea nchini China wakiwa katika picha ya pamoja |
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hannelore Manyanga (aliyekaa) katika picha ya pamoja na 'wasafiri' |
Kiongozi wa Msafara, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mariam Mwanzalima akitoa neno la shukrani kwa niaba ya 'wasafiri' |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni