Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Oktoba 2017

UHAMIAJI WAFANYA USAFI NA KUFARIJI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala aliongoza watumishi wa idara hiyo kwenye zoezi la usafi na kuwafariji wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke.
Zoezi hilo lililofanyika leo jumamosi ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali la kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. 


Baada ya kukamilisha zoezi la usafi, Dkt. Makakala akiongozwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Temeke Dkt. Amaani K. Malima walielekea katika wodi ya watoto na wodi ya kina mama wajawazito na kugawa vifaa na zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafariji wagonjwa hao.

Aidha, Dkt. Makakala alikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa uongozi wa hospitali kwa ajili ya kuimarisha afya na usafi hospitalini hapo.


Vifaa na zawadi mbalimbali zilizogawiwa kwa wagonjwa hospitalini hapo zilikuwa na jumla ya thamani ya shilingi milioni nane.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. A.P Makakala akivaa 'gloves' tayari kwa ajili ya kuzindua rasmi zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke ikiwa kutekeleza agizo la Serikali la kufanaya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Kamishna Jenerali wa  Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Jackoson Lyaniva (kulia) na Kamishna wa Uhamiaji Salum Mwinchumu (kushoto) wakijiandaa kuanza zoezi la usafi.

Watumishi wa Uhamiaji wakijiandaa kuanza zoezi la usafi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akiwaongoza watumishi kuelekea maeneo mbalimbali ya kufanya usafi katika Hospitali ya Temeke

makamishina wa Uhamiaji wakishiriki katika zoezi la usafi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisafisha mtaro katika Hospitali ya Temeke

Kamishna wa Uhamiaji Salum Mwinchumu (kulia) na Mrakibu msaidizi wa Uhamiaji Paul Msele (kushoto) wakishiriki katika zoezi la usafi.

Mganga Mkuu wa Hopitali ya Temeke Dkt. Amaan Malima akishiriki vyema katika zoezi la usafi.

Maafisa na Askari wa Uhamiaji wakishiri katika zoezi la usafi.


Askari wa Uhamiaji wakifanya usafi.

Askari wa Uhamiaji wakifanya usafi.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dkt. Amaan K. Malima akishiriki kwenye zoezi la usafi pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akisafisha mtaro.

Kamishna wa Uhamiji Utawala na Fedha 

Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Samwel Magweiga akishiriki zoezi la usafi 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji akikabidhi vifaa vya usafi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke

kamishna jenerali wa uhamiaji akisaidi kitabu cha wageni katika hospital ya Temekekamishna jenerali wa uhamiaji akimkabidhi mganga mkuu wa hospitali ya Temeke  jarida la uhamiaji 

kamishna generali wa uhamiaji washukuru watumishi kwa kushiriki vyema katika zoezi la usafi lililofanyika Hospitali ya Temeke

Mmoja wa viongozi katika hospitali ya Temeke akizungumza na watumishi wa idara ya uhamiaji wakiongozwa na kamishna jenerali wa uhamiaji Dr Anna Makakalawagonjwa wakisoma vijarida vya uhamiaji walivyogawiwa na watumishi wa idara ya uhamiaji katika hospitali ya Temeke

Mganga mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amaan Malima akiwatembeza katika maeneo mbalimbali ya hospitali  watumishi wa idara ya uhamiaji wakiongozwa na kamishna jenerali wa uhamiaji Dr Anna Makakala

Zawadi mbalimbali zikikabidhiwa kwa wagonjwa katika hospitali ya Temeke


Kamishna jenerali wa uhamiaji Dr Anna Makakala aimkabidhi zawadi mgonjwa katika wilaya ya Temeke


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni