Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Khamis amefanya ziara kutembelea ofisi za Uhamiaji Makao Makuu pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma siku ya Alhamis tarehe 24 Juni, 2021.
Mhe. Khamis akiwa Uhamiaji Makao Makuu eneo la Uzunguni, alipata wasaa wa kuongea na Maafisa, Askari na Watumishi wa Uhamiaji Makao Makuu na kuwataka kuchapa kazi kwa weledi, kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuzingatia sheria za nchi katika kuwahudumia raia wa Tanzania na Wageni.
Awali, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makalala akisoma taarifa ya Utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji alisema kwamba anaishukuru serikali kwa kuwapandisha vyeo maafisa, askari na watumishi wa kada ya kiraia zaidi ya 1000.
Naibu waziri baadae alielekea eneo linapojengwa jengo la Uhamiaji Makao Makuu na kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo na kuwataka wakandarasi kuharakisha ujenzi huo ikibidi kufanya kazi usiku na mchana ili kabla ya kuisha mwaka huu basi jengo hilo lianze kutumika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Khamis Hamza Khamis kutembelea idara ya Uhamiaji toka ateuliwe kuwa naibu waziri mwishoni mwa mwaka jana na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo mabadiliko yaliyofanya na Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu hassan hayakuathiri wizara ya mambo ya ndani.
Dkt. Anna Makakala akisoma taarifa ya Utendaji kazi wa Idara ya Uhamiaji mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Khamis Hamza Khamis |
Baadhi ya Maafisa, Askari na watumishi wa Idara ya Uhamiaji wakimsikiliza Mhe. Khamis wakati akiongea nao nje ya jengo ya ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma |
Naibu Waziri Mhe. Khamis Hamza Khamis akiandika katika kumbukumbu zake wakati akiskiliza taarifa kutoka kwa Dkt. Makakala |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Khamis akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji Dodoma |
Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha) Hamza Ismail Shaabani akitoa taarifa ya maendeleo wa jengo la Uhamiaji Makao Makuu jijini Dodoma |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni