Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu mapema wiki hii atembelea vipenyo mbali mbali katika Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba ili kujionea mazingira halisi pamoja na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wakushirikiana na Idara ya Uhamiaji katika kutoa taarifa kwa Wahamiaji wasiofuata sheria za Uhamiaji.
Akizungumza
na Wananchi wanaoishi pembezoni mwa vipenyo vya mto wa kuwa na Mkia wa ng’ombe huko
Kaskazini Pemba aliwataka wananchi kushiriki katika kuimarisha ulinzi kwenye vipenyo
kwa kutoa taarifa kwa Idara ya Uhamiaji kuhusu chombo chochote kinachokusudia
au kuonekana katika eneo hilo ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Kamishna
Sururu aliwafahamisha Wananchi hao athari za Uhamiaji haramu ikiwa ni pamoja na
kuhatarisha usalama wa nchi na Serikali kukosa mapato yatokanayo na malipo ya
visa.
Aidha
Wananchi walitaka kupatiwa elimu zaidi ya Uhamiaji ili wawe na uwezo wa kuwabaini
Wahamiaji Haramu katika maeneo yao. Wananchi hao waliahidi kutoa mashirikiano
na Idara ya Uhamiaji.
Nae Sheha
wa Shehia ya Gando Maalim Karim Mangunja alibainisha kuwa hakuna vyombo vya kigeni
vinavyoingia katika vipenyo hivyo hata hivyo aliahidi pale ikitokea chombo
chochote ikitakachotiliwa shaka ataijuilisha Idara ya Uhamiaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni