Visitors
25 Juni 2021
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI, DKT. A.P. MAKAKALA, AFUNGUA WARSHA KUHUSU USALAMA WA MIPAKA KWA NJIA YA MTANDAO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji DKT. A. P. Makakala mapema wiki hii afungua warsha kuhusu Usalama wa Mipaka, warsha hiyo inayoendeshwa katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Moshi, ilifunguliwa na Kamishna Jenerali kwa njia ya mtandao akiwa Zanzibar.
Katika hotuba yake Dkt. Makakala alifahamisha kuwa usalama wa mipaka lazima upewe kipaumbele hasa kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo yanachangia uhalifu unaovuka mipaka (Transnational Organized Crimes) duniani kote.
Dkt. Makakala aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuwa makini na kuzingatia mafunzo watakayopatiwa ili waweze kuwafundisha wenzao ambao hawakupata fursa ya kushiriki mafunzo hayo pamoja na kuwataka kutumia mbinu mpya walizofundishwa katika marsha hiyo katika kudhibiti Uhalifu unaovuka mipaka.
Maafisa 32 walioshiriki katika warsha hiyo kutoka vituo mbali mbali vya kuingilia na kutokea watu nchini kutoka Tanzania Bara na Zanzibar walijifunza ukaguzi wa nyaraka, mienendo na mabadiliko ya mbinu za kudhibiti ugaidi, dawa za kulevya, umuhimu wa intelijensia katika kusimamia ulinzi na usalama wa mipaka pamoja na matumizi ya mifumo mbalimbali ya Uhamiaji.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni