Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

11 Desemba 2021

UHAMIAJI WALIVYOIPAMBA SHEREHE YA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU.

Na Konstebo Amani Mbwaga

Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mara ya kwanza alikagua Gadi ya Jeshi la Uhamiaji wakati wa Sherehe ya Maadhimisho ya kutimiza Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara.

Sherehe hizo zimefanyika  tarehe 09 Disemba 2021, katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam ambapo Uhamiaji imeandika historia kwa mara ya kwanza chini ya kiongozi hodari Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini  Dkt. Anna Makakala kushiriki katika gwaride la maadhimisho hayo wakishirikiana na Majeshi mengine hapa nchini ambayo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan alipowasili katika uwanja huo ulipigwa wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki ambao uliambata na mizinga 21 kisha alianza kukagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwa ajili maadhimisho hayo ambapo gwaride hilo lilikuwa na gadi mbalimbali zilizoundwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini zikiwemo gadi za Jeshi la Uhamiaji.

Baada ya ukaguzi, kiongozi mkuu huyo wa nchi alielekea jukwaa kuu kuungana na viongozi wengine kisha gwaride lilianza kupita kwa mwendo wa pole na haraka.

Sherehe hizo zilitawaliwa na kila aina ya hamasa huku umati mkubwa wa wananchi wakifika katika uwanja wa uhuru, wakivutiwa na matukio ya aina mbalimbali yaliyoanza kushuhudiwa tangu saa mbili asubuhi na kuendelea hadi nyakati za saa nane mchana.

Wakati vikosi  vikihitimisha gwaride na kutoka eneo la uwanja, vikosi vya makomandoo wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakiwa na mabegi mgongoni yanayokisiwa kuwa na kilo zaidi ya 30 nao walipita mbele ya Mhe. Rais na baadae kuendelea na maonesho mengine yakiwemo ya ndege vita na uokozi pamoja na vifaa vita vingine ili kuonesha kwamba nchi yetu ipo salama wakati wote.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa ambae alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo, alisema kwa namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi ni ushuhuda tosha kwamba taifa hili limesafiiri miaka 60 ya uhuru katika njia ya amani na utulivu.

Rais Samia aliongoza maadhimisho haya, ikiwa ni ya kwanza katika utawala wake na ya kwanza kwa Jeshi la Uhamiaji kushiriki tangu Uhuru.

Aidha Mhe. Rais aliungwa mkono na marais wengine kutoka ukanda wa Afrika, ikiwamo Msumbiji, Rwanda, Comoro na Kenya.

Rais Samia kwenye maadhimisho hayo hakuwa na hotuba ndefu mbali ya kuwatambulisha wageni wake lakini alitumia muda mwingi kwenye hotuba aliyotoa  usiku siku moja kabla ya maadhimisho  kutaja mafanikio yaliyofikiwa tangu taifa hili lilipopeperusha kwa mara ya kwanza bendera yake mnamo Disemba 9, 1961.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gadi ya Uhamiaji katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaamRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalima Wananchi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam tarehe 9 Disemba 2021

Gadi ya Jeshi la Uhamiaji Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyata akiwasili katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam tarehe 9 Disemba 2021


Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwasili katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam tarehe 9 Disemba 2021

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala

Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akisalimiana na baadhi ya viongozi wa serikali na wageni waalikwa katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam tarehe 9 Disemba 2021
Baadhi ya Makamishna wa Uhamiaji Pichani walihudhuria sherehe hizo

Baadhi ya Maofisa na Askari wa Uhamiaji walihudhuria sherehe hizo


Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Hamza Shaban (kulia) akiwa na Mkuu wa chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Moshi  Kamishna Abdalah Towo wakifuatilia kwa makini maonesho yanayoendelea ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru.Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Masoud Sururu akiwa katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru

Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga akifuatilia kwa makini maonesho mbalimbali ya Miaka 60 ya Uhuru yaliyokuwa yakiendelea katika uwanja wa Uhuru tarehe 09 Disemba 2021
Askari wa JWTZ wakiwa katika moja ya onesho katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru 

Askari wa JWTZ wakiwa katika moja ya onesho katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru 


Askari wa JWTZ wakiwa katika moja ya onesho katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru 

Askari wa JWTZ wakiwa katika moja ya onesho katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru 

Askari wa JWTZ wakiwa katika moja ya onesho katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru Gadi za Uhamiaji zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru

Gadi za Uhamiaji zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa heshima wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru
Gadi za Polisi zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru

Gadi za JKT zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru

Gadi za JWTZ zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru

Gadi za JWTZ zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru


Gadi za JWTZ zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya UhuruGadi za Magereza  zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru


Gadi za Magereza  zikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru(Picha zote na Konstebo wa Uhamiaji Amani Mbwaga tarehe 9 Disemba 2021)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni