Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

27 Desemba 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: UHAMIAJI MKOA WA DODOMA WALIVYOSHIRIKI USAFI SAMBAMBA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Dkt. Binilith Mahenge alivyoshiriki kufanya usafi katika Mtaa wa Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini siku ya Jumamosi katika Kampeni ya Usafi wa Mji ambapo Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walishiriki wakiongozwa na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Naibu Kamishna wa Uhamiaji P.J. Kundy.

Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge akifanya usafi katika Kampeni ya Usafi wa Mji wa Dodoma.

Afisa Uhamiaji Mkoa Dodoma; Naibu Kamishna wa Uhamiaji P. J. Kundy akizungumza na waandishi wa Habari baada ya zoezi la Usafi wa Mji wa Dodoma.
Maafisa Uhamiaji wa Dodoma wakifanya Usafi katika Kampeni ya Usaifi wa Mji wa Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya zoezi la Usafi wa Mji wa Dodoma

Baadhi ya Wananchi wa Dodoma walioshiriki katika siku ya usafi.KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR AWAASA MAAFISA UHAMIAJI PEMBA KUFANYA KAZI KWA WELEDI


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu akizungumza na Watumishi wa Uhamiaji katika Ofisi ya Uhamiaji Kaskazini Pemba.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu amewataka Askari na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kuweza kutekeleza vyema majukumu yao ya msingi ya kusimamia na kudhibiti Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Watu Nchini wakati wa majumuisho ya ku
hitimisha ziara yake katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba iliyoanza tarehe 18 – 21 Disemba, 2017. 

Akizungumza na Watumishi katika ziara hiyo Kamishna Sururu alisema,“Ili kuimarisha utendaji wetu ni vyema kuacha kufanya kazi kwa mazowea na muda wote, tutoe huduma za Uhamiaji bila ya Upendeleo, Unyanyasaji au Ucheleshwaji usio wa lazima. Tutumie lugha nzuri na tutekeleze kwa vitendo dhana ya kumjali Mteja katika misingi ya sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma''
.
Aidha, katika ziara hiyo, Kamishna Sururu alifika katika vipenyo na Bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa maeneo hayo, kwa shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na biashara haramu ya kuingiza Wahamaiji haramu nchini wakitokea Nchi mbali mbali tunazopakana nazo kwa upande wa bahari ya Hindi. Kisiwa cha Pemba kinasemekana kuwa na Bandari bubu zaidi ya mia tatu (300) ambazo zinatumiwa na wahalifu hao kusafirisha Wahamiaji na magendo, Wilaya za Micheweni, Wete na Mkoani ndizo zizoathiriwa zaidi na vitendo hivyo dhalimu.


Kadhalika, Kamishna Sururu alimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis Othman, Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Pemba na aliongea na baadhi ya wananchi ambapo alisikiliza kero zao na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akipokea salamu kutoka kwa Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwasili Ofisi hapo kwa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Said M. Samaki akichangia hoja katika kikao cha pamoja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.Sheha wa Shehia ya Shumba Mjini, Bi. Rahma Mohamed Shaame (katikati) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto kwake), kuhusu matumizi ya Bandari bubu Shumba Mjini inayotumiwa na wakaazi wengi wa Wilaya ya Micheweni kufanya safari zao za kibiashara kwenda Visiwa vya Mombasa Kenya.

Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za Idara ya Uhamiaji Nchini.


Tumbe ni mojawapo ya Bandari Bubu zilizopo ndani ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

22 Desemba 2017

KAMISHNA WA UHAMIAJI(ZANZIBAR) AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu (wa pili kushoto) akipokea salamu za Wananchi wa Shumba Mjini, akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 20 Disemba 2017, alipotembelea Bandari Bubu iliyopo Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo ni maarufu kwa shughuli za Uvuvi na Biashara.  

Mkuu wa Diko “Bandari Bubu” ya Shumba mjini,Bwana Hussein Rashid Omar, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar) Johari M. Sururu baadhi ya Majahazi (hayapo pichani) yanayofanya safari zake kupitia Bandari bubu hiyo.wakati alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 Disemba, 2017.

Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za Idara ya Uhamiaji Nchini.
Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu za Kiuyu na Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali, Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.

21 Desemba 2017

SALAMU NA UJUMBE WA KRISMASI KWA WATANZANIA KUTOKA KWA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI

Kamishna Jenerali Wa Uhamiaji kwa niaba ya Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji Tanzania anawatakia Watanzania Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya wa 2018.

Aidha anatoa wito kwa wananchi wote hasa waishio maeneo ya mipakani kutoa taarifa kwa Idara ya Uhamiaji ama Vyombo vingine vya Dola pale wanapoona makundi ya watu wakipita katika maeneo yao, kwani Wahamiaji Haramu wanaweza kujipenyeza na kuingia nchini kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.

Pia anawakumbusha Watanzania kuwa, Uvushaji, ama Usafirishaji, Uhifadhi wa Wahamiaji Haramu au Usaidizi wa aina yoyote  kwa Wahamiaji ni Kosa la Jinai kwa Mujibu wa Sheria ya Uhamiaji


20 Desemba 2017

ZIARA YA KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR KATIKA MKOA WA KUSINI PEMBA

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 18-19 Disemba 2017 katika Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni muendelezo wa ziara za kukagua utendaji kazi wa maafisa uhamiaji ili kuhakikisha wananchi na wageni wanapata huduma kwa wakati.

Akiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, alikagua vitabu vya Hati za kusafiria zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi na kuwasisitiza Maofisa Uhamiaji katika utoaji wa Hati hizo wazingatie vyema Sheria na Taratibu zilizopo ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu aliwanasihi Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba kuzingatia maadili ya kazi, pamoja na kutilia mkazo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

“Naelewa tupo kwenye utandawazi, lakini narudia kuwasihi matumizi ya Mitandao ya kijamii itumike kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Serikali, pia mjiepushe na utoaji wa Siri na Taarifa za serikali, ni mwiko kutoa taarifa yoyote, fuateni Sheria na Taratibu tulizowekewa.”  alisema Kamishna Sururu.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis alipokuwa akichangia hoja wakati wa kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini Pemba siku ya tarehe 19 Disemba, 2017. Alisema “Ongezeko la Bandari Bubu ndani ya Wilaya ya Mkoani ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu. Tunazo takriban Bandari bubu 103, tunaomba Idara itupatie gari la kufanyia doria katika maeneo hayo”. Kwa upande wake Kamishna Sururu aliahidi kulifanyia kazi ombi mapema iwezekanavyo.

Katika ziara hiyo, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu ambaye aliambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, alikagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia za Kengeja na Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba, kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii, ambazo hutumika kama vipenyo kwa watu kuingia na kutoka visiwani humo kinyume na taratibu za Uhamiaji. 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia ya Kengeja, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto) akikagua baadhi ya magari chakavu yaliyopo katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, yanayosubiri kupigwa mnada baada ya kukamilika kwa taratibu za uuzaji wa Mali za Serikali, wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 – 19 Disemba, 2017. Pamoja na kutembelea maeneo mbali mbali ya utendaji kazi Mkoani humo ikiwemo Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wesha iliyopo Chake Chake na Bandari bubu kadhaa. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi. 
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba.  

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Juma A. Khamis (aliesimama) akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (hayupo pichani) na Watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko Mkoa wa Kusini Pemba siku ya tarehe 19 Disemba, 2017

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akikagua kitabu cha utoaji wa Hati za Dharura za Kusafiria “ETD” katika Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mkoani, zinazotolewa kwa Watanzania wanaohitaji kusafiri nje ya Nchi. 


Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akitoa nasaha zake kwa Maafisa, Askari na watumishi Raia wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani humo Leo tarehe 19 Disemba, 2017.

Sheha wa Shehia ya Kengeja, Mohamed Kassim Mohamed (kulia) akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (katikati) na Maafisa waandamizi wa Uhamiaji alioambatana nao, Bandari bubu ya Mbuyuni inayotumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa mahitaji mbali mbali ikiwemo uvuvi.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa Shehia ya Muwambe, Kusini Magharibi mwa kisiwa cha Pemba.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Hassan A. Ramadhan (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) kuhusu mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inavyosaidia kurahisisha mawasiliano na utendajikazi katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba.  

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdi Bulushi akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) na Maafisa Uhamiaji aliombatana nao, matunzo na usafi wa mazingira katika nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji, zilizoko eneo la Ndugukitu, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba. 

Nyumba za makazi ya Askari na Maafisa Uhamiaji zilizopo Ndugukitu Chakechake zilifunguliwa rasmi na Mhe. Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi mapema mwezi Januari, 2017.

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AFANYA KIKAO NA WATUMISHI NA KUWATAKIA SIKUKUU NJEMA


  • Amewakumbusha Maafisa kufanya kazi kwa juhudi na weledi ili kuepusha malalamiko kwa wananchi.
  • Amewatakia Sikukuu Njema ya Krismasi na Mwaka Mpya na kuwataka kujipanga katika mwaka ujao ili kuyatimiza malengo yaliyopo na kuyafikia matarajio ya wananchi na raia wa kigeni wanaofika kuhudumiwa.

  • Atoa zawadi ya sikukuu ambayo ni kikombe (Mug) kwa kila afisa/Mtumishi ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

Afande Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, katika Kikao cha Watumishi wote  jana mchana, Makao Makuu ya Uhamiaji.  Aliyeketi  kulia kwake ni Kamishna wa Uhamiaji (Sheria), Hannelore Morgan Manyanga na kushoto kwake ni Kamishna wa Uhamiaji (Paspoti na Uraia), Gerald Kihinga. Katika kikao hicho Afande Jenerali aliwatakia watumishi wote wa Uhamiaji, sherehe njema za Krismasi na Mwaka mpya na kukumbusha weledi na na uadilifu katika utendaji kazi.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  
Afande Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala akitoa zawadi ya kikombe kwa Mfawidhi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Uhamiaji Kijichi,Naibu Kamishina wa Uhamiaji Lusungu Ngailo wakati wa kikao cha Maafisa, askari na Watumishi raia wote wa Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere,  jana mchana, Makao Makuu ya Uhamiaji.  Zawadi hiyo ya vikombe ilitolewa kwa wajumbe wote waliohudhuria kikao kwa lengo la Kamishna Jenerali kuwatakia sherehe njema za Krismasi na Mwaka mpya wana Uhamiaji wote nchini na walioko vituo vya  ng'ambo ya nchi.  

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji Waandamizi walioshiriki kikao cha Kamishna Jenerali na Watumishi wote wa Uhamiaji Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere jana . Katika Kakao hicho Afande Jenerali aliwakumbusha watumishi wote kutenda kazi kwa weledi na uadilifu.


Baadhi ya Wafawidhi wa Vitengo vya Makao walioshiriki kikao cha Kamishna Jenerali na Watumishi wote wa Uhamiaji Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere jana . Katika Kakao hicho Afande Jenerali aliwakumbusha watumishi wote kutenda kazi kwa weledi na uadilifu.15 Desemba 2017

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AKUTANA NA WATANGULIZI WAKE

  • Achota busara hekima na ujuzi kutoka kwa wastaafu.
  • Wastaafu wamfagilia kwa utendaji kazi uliotukuka.
  • Wasema kwa sasa Idara inatekeleza kauli mbiu ya Mhe. Rais ya 'HAPA KAZI TU'.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amepata fursa ya kukutana na viongozi waandamizi wastaafu waliowahi kuiongoza Idara ya Uhamiaji katika kikao cha pamoja kilichofanyika leo tarehe 15 Disemba 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa TEC, Kurasini jijini Dar es Salaam. 

Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kupokea ushauri, kubadilishana mawazo na kupeana uzoefu baina ya viongozi wa sasa na viongozi waandamizi wastaafu wa Idara ya Uhamiaji.

Akifungua kikao hicho, Dkt Makakala alielezea furaha yake kwa kupata fursa ya kipekee kwa  kukutana na wazee ambao ni waanzilishi wa Idara ya Uhamiaji, na kuwaomba waweze kutoa ushauri wao na kubadilishana uzoefu na viongozi wa sasa wa Idara, juu ya masuala mbalimbali kwa nia ya kuongeza ufanisi na kutatua changamoto ambazo Idara imekuwa ikikabiliana nazo.

"Nina furaha kubwa sana yaani leo, sijui nieleze vipi. Leo nipo na Wakuu wangu walionilea idarani hadi na mimi nimekuwa Mkuu wa Idara. Ni jambo kubwa sana mmenifanyia kwa kukubali kuja hapa ili mnifunde mimi na wenzangu. Nawashukuru sana." alisema Kamishna Jenerali wa Uhamiaji wakati akiwakaribisha wastaafu hao.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wastaaafu, Mkurugenzi mstaafu wa Uhamiaji, Kinemo Kihomano alimpongeza Dkt Makakala kwa kuteuliwa kuwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, na kumtaka kuendeleza yale mazuri yaliyoanzishwa na viongozi wastaafu na kuendeleza ubunifu na utekelezaji wa mipango mbalimbali aliyokwishaanza kuitekeleza kulingana na mahitaji ya wakati wa sasa.

Kwa upande wake Kamishna Ally Mnyika, mbali ya kumpongeza Dkt Makakala, alimshauri kufanya kazi bila woga wala upendeleo wa aina yoyote, kutekeleza na kusimamia maamuzi mbalimbali atakayokuwa akiyafanya ili mradi amezingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

Katika kikao hicho, viongozi mbalimbali wastaafu walipata fursa ya kutoa uzoefu wao juu ya masuala mbalimbali ya kiuhamiaji na namna walivyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali walizokutana nazo wakati wa uongozi wao  kwa nia ya kuboresha utendaji wa Idara ya Uhamiaji.

Ikumbukwe kwamba Idara ya Uhamiaji imepitia mabadiliko kadhaa ya vyeo vya uongozi ambapo hapo awali Mkuu wa idara alikuwa akijulikana kama Mkurugenzi wa Uhamiaji, baadae Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na sasa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji.

Aidha katika Kikao hicho walihudhuria Wakurugenzi Wastaafu wa Uhamiaji Ally A. Mnyika, Judith Vicky Mtawali, Kinemo W. D. Kihomano na Magnus P. J Ulungi. Wengine ni Masauni Yusuf Masauni, Makame Usi Ali, na Ali Khamis Ali kwa upande wa Zanzibar. Kadhalika Makamishna Piniel O. Mgonja, Donald S. B. Ndagula, John Choma, Francis Kibula, Cuthbert Samba, Faustina B. Rutaihwa, Barikiel Shayo, George J. Kashwende pamaoja na Makamishna waliopo Madarakani kwa sasa na Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Zanzibar pamoja na baadhi ya Mikoa walihudhuria.

Wakurugenzi wa Uhamiaji Wastaafu Ally A. Mnyika (kulia), Judith Mtawali (katikati) wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. A. P. Makakala akizungumza jambo wakati wa kikao kazi na watangulizi wake kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.

Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Piniel O. Mgonja akichangia jambo katika kikao cha pamoja baina ya Viongozi Waandamizi Wastaafu wa Idara ya Uhamiaji na Viongozi Waandamizi waliopo madarakani.

Mkurugenzi Mkuu Mstaafu  wa Uhamiaji Zanzibar Masauni Yusuf Masauni akichangia hoja wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kazi
Mkurugenzi Mstaafu wa Uhamiaji Judith Vicky Mtawali akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kazi baina ya Viongozi Waandamizi wastaafu wa Idara ya Uhamiaji na Viongozi Waandamizi wa Idara waliopo madarakani.

Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Uhamiaji Kinemo Kihomano akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kazi baina ya Viongozi Waandamizi wastaafu wa Idara ya Uhamiaji na Viongozi Waandamizi wa Idara waliopo madarakani.

Picha ya pamoja ya Viongozi waandamizi wa  Idara ya Uhamiaji waliopo madarakani na Viongozi Waandamizi wastaafu wa Idara hiyo, wakati waliposhiriki katika kikao cha kubadilishana mawazo na uzoefu kilichoitishwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt.  Anna Makakala.

Kamishna Wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu akizungumza wakati wa Kikao hicho.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Uhamiaji Mzee Ally Mnyika.

Mamishna wa Uhamiaji Piniel O. Mgonja (kulia), John Choma (katikati) na Cuthbert Samba (kushoto) wakifuatilia yanayojili katika kikao hicho.

Manaibu Kamaishna wa Uhamiaji George J. Kashwende (kushoto), Francis Kibula (wapili kushoto), Faustina B. Rutaihwa na Barikieli Shayo wakifuatilia kikao hicho

Makamishna wa Uhamiaji Gerald Kihinga, Maurice D. Kitinusa, Mwinchum H. Salum na Mary Palmer wakifuatilia yanayojili katika kikao hicho.

Kamishna wa Uhamiaji Dkt. A. P. Makakala na Mkurugenzi Mstaafu wa Uhamiaji Judith Mtawali wakifuatilia yanayojili katika kikao hicho.Makamishna wa Uhamaiji Kutoka kushoto Hannelore M. Mnyanga, Samwel R. Magweiga, Gerald Kihinga, na Maurice Kitinusa wakifuatilia yanayojili kwenye kikao hicho.

Makamishna wa Uhamiaji Maurice Kitinusa (kushoto), Mchinchum H. Salum(katikati) na Mary Palmer  (kulia) wakifuatilia yanayojili katika kikao hicho. 

Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald S. B. Ndagula akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Cuthbert Samba akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu John Choma  akizungumza jambo kwenye kikao hicho.

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mstaafu Magnus P. J. Ulungi  akizungumza kwenye kikao hicho cha kubadilishana uzoefu na ushauri baina ya Viongozi Waandamizi Wastaafu na waliopo Madarakani.

Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji waliopo Madarakani na Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja kabala ya kunza kikao hicho.

Mkurugenzi  wa Uhamiaji Mstaafu Ally A. Mnyika akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Kamishna wa Uhamiaji Mstaafu Donald S. B. Ndagula akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Kamishna wa Uhamiaji Donald S. B. Ndagula akichangia jambo kwenye kikao hicho

Mkurugenzi wa Uhamiaji Mstaafu  wa Zanzibar Masauni Yusuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari baada kikao hicho.

Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Uthumishi, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Joseph Francis Kasike  akifuatilia jambo katika kikao hicho.

Kamaishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. A. P. Makakala akizungumza katika kiakao hicho.

Makamaishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari Sururu (kulia) na Makamishna wengine wakifuatilia kikao hicho