Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa
wa Kaskazini Unguja tarehe 06 Disemba, 2017.
Katika
ziara hiyo, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu amewaasa
watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuzingatia Maadili ya
kazi, Heshima na Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi uliotukuka.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu
Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin akiwasilisha kwa Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari Masoud Sururu, taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hiyo kuanzia Julai
hadi Novemba, 2017, alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko la makusanyo ya
maduhuli ya Serikali kwa kipindi hicho ambapo jumla ya Dola za Kimarekani 34,000/- zilikusanywa.
Akiwa
katika Bandari ya Mkokotoni, Kamishna Sururu alipokewa na Mkuu wa Bandari ya Mkokotoni,
Bwana Ahmed Salim Said ambapo alioneshwa
eneo linalotumiwa na baadhi ya Manahodha kushusha abiria kinyume na utaratibu
wa Bandari hiyo, wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendaji kazi
wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 |
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (juu), akiwaasa watumishi wa Idara
ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuzingatia Maadili ya kazi, Heshima na
Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi uliotukuka. Alitoa nasha hizo
leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo.
Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa
Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin na kushoto ni Afisa Utumishi, Mrakibu wa Uhamiaji,
Ali J. Abdulkadir.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni