Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

22 Desemba 2017

KAMISHNA WA UHAMIAJI(ZANZIBAR) AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu (wa pili kushoto) akipokea salamu za Wananchi wa Shumba Mjini, akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 20 Disemba 2017, alipotembelea Bandari Bubu iliyopo Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo ni maarufu kwa shughuli za Uvuvi na Biashara.  

Mkuu wa Diko “Bandari Bubu” ya Shumba mjini,Bwana Hussein Rashid Omar, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar) Johari M. Sururu baadhi ya Majahazi (hayapo pichani) yanayofanya safari zake kupitia Bandari bubu hiyo.wakati alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 Disemba, 2017.

Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za Idara ya Uhamiaji Nchini.
Kamishna wa Uhamiaji (Zanzibar), Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu za Kiuyu na Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali, Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni