Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

20 Desemba 2017

KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI AFANYA KIKAO NA WATUMISHI NA KUWATAKIA SIKUKUU NJEMA


  • Amewakumbusha Maafisa kufanya kazi kwa juhudi na weledi ili kuepusha malalamiko kwa wananchi.
  • Amewatakia Sikukuu Njema ya Krismasi na Mwaka Mpya na kuwataka kujipanga katika mwaka ujao ili kuyatimiza malengo yaliyopo na kuyafikia matarajio ya wananchi na raia wa kigeni wanaofika kuhudumiwa.

  • Atoa zawadi ya sikukuu ambayo ni kikombe (Mug) kwa kila afisa/Mtumishi ndani ya mkoa wa Dar es salaam.

Afande Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, katika Kikao cha Watumishi wote  jana mchana, Makao Makuu ya Uhamiaji.  Aliyeketi  kulia kwake ni Kamishna wa Uhamiaji (Sheria), Hannelore Morgan Manyanga na kushoto kwake ni Kamishna wa Uhamiaji (Paspoti na Uraia), Gerald Kihinga. Katika kikao hicho Afande Jenerali aliwatakia watumishi wote wa Uhamiaji, sherehe njema za Krismasi na Mwaka mpya na kukumbusha weledi na na uadilifu katika utendaji kazi.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                  
Afande Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala akitoa zawadi ya kikombe kwa Mfawidhi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Uhamiaji Kijichi,Naibu Kamishina wa Uhamiaji Lusungu Ngailo wakati wa kikao cha Maafisa, askari na Watumishi raia wote wa Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere,  jana mchana, Makao Makuu ya Uhamiaji.  Zawadi hiyo ya vikombe ilitolewa kwa wajumbe wote waliohudhuria kikao kwa lengo la Kamishna Jenerali kuwatakia sherehe njema za Krismasi na Mwaka mpya wana Uhamiaji wote nchini na walioko vituo vya  ng'ambo ya nchi.  

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji Waandamizi walioshiriki kikao cha Kamishna Jenerali na Watumishi wote wa Uhamiaji Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere jana . Katika Kakao hicho Afande Jenerali aliwakumbusha watumishi wote kutenda kazi kwa weledi na uadilifu.


Baadhi ya Wafawidhi wa Vitengo vya Makao walioshiriki kikao cha Kamishna Jenerali na Watumishi wote wa Uhamiaji Makao Makuu, Mkoa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere jana . Katika Kakao hicho Afande Jenerali aliwakumbusha watumishi wote kutenda kazi kwa weledi na uadilifu.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni