Na. Amani Mbwaga, Dar es Salaam.
Jeshi la Uhamiaji Nchini limeishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa namna ya kipekee anavyoliwezesha Jeshi la Uhamiaji kulijengea uwezo na hatimae kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.
Hayo yamesemwa jana tarehe 03 Februari 2023 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania (CGI) Dkt. Anna Makakala wakati akiongea na Maofisa Askari, na Watumishi raia katika ziara yake ya Kikazi Jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo inahusu uendeshwaji wa Operesheni
Maalumu itakayoanza hivi karibuni sanjari na kukagua Utendaji kazi wa Maofisa
Askari na Watumishi raia kwa mwaka 2022/2023.
Katika ziara hiyo CGI Dkt. Anna Makakala alitembelea Ofisi ya Uhamiaji Mkoa, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) Kituo cha Uchapaji Nyaraka Kijichi Printing Unit (KPU), Kiwanda cha Ushonaji nguo kilichopo Kijichi, Uhamiaji band sanjari na Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kigamboni.
Aidha Dkt. Makakala ametoa maelekezo kwa Viongozi wengine waandamizi wa Jeshi la Uhamiaji kuendelea na ziara kama hiyo katika Mikoa mingine yote Nchini ili kuangalia na kuhimiza utendaji kazi katika ofisi za Mikoa, Wilaya na Vituo vya kuingilia na kutoka Nchini.
Katika ziara hizo Viongozi hao watapata nafasi ya kusikiliza changamoto za utendaji kazi pamoja na matatizo mbalimbali ya Maofisa, Askari na watumishi raia na hatimae kuyatafutia ufumbuzi.
Akiongea kwa wakati tofauti tofauti na Maafisa, Askari na Watumishi raia katika shemu zote alizotembelea, Kamishna Jenerali Dkt. Anna Makakala amesisitiza zaidi kuendelea kufanya kazi kwa Ubunifu, Utii, Uhodari, Uzalendo, na Weledi wa Hali ya juu ili kufikia Dira ya Uhamiaji ya Kuwa Taasisi yenye utendaji bora inayotoa huduma za Uhamiaji zenye kukidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa kwa manufaa ya Kizazi cha sasa na baadae.
"Ni imani yangu kwamba mtaendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa lengo la kuleta tija kwa Jeshi na Taifa kwa ujumla" Alisema CGI Dkt. Makakala.
Katika suala la upandishwaji vyeo CGI Dkt. Anna Makakala alisema serikali kwa mwaka fedha 2020/2021 iliwapandisha madaraja mbalimbali Maofisa, Askari na Watumishi raia zaidi ya 1000 aidha katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya watumishi 182 walipandishwa vyeo .
Hata hivyo serikali kupitia ikama za mwaka 2022/2023 na 2023/2024 inataraji kuwapandisha vyeo zaidi ya Maofisa, Askari na Watumishi raia 1200 ambao wamekidhi vigezo vya kimuundo, kupitia hili Jeshi la Uhamiaji linaendelea kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa vibali vya kuwapandisha vyeo watumishi sambamba na kuboresha maslahi yao.
HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiwasili katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam. |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Peter Mwitwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Maofisa na Askari wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam |
Maofisa na Askari wa Kituo cha Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere wakifuatilia kwa kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (Hayupo Pichani) |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Maofisa na Askari wa Kituo cha Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (Kushoto) akikagua mradi wa Kiwanda cha Uhamiaji cha Ushonaji nguo kilichopo Kijichi Jijini Dar esalaaam. |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akikagua nyaraka zinazochapishwa na Kiwanda cha Uhamiaji cha Uchapaji Kijichi Printing Unit (KPU) |
Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kigamboni Mrakibu wa Uhamiaji Christian Mndeme akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (Hayupo Pichani) |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa, Askari na Watumishi raia wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kigamboni. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni