Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

25 Novemba 2020

Uhamiaji Kagera yatoa Elimu kwa Umma katika Uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Sheria.

Kagera

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera mapema wiki hii imeshiriki katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma za Sheria nchini inayoendelea Mkoani humo Wilayani Karagwe katika Viwanja vya stendi ya Omurushaka villivyopo kata ya Bugene.

Uzinduzi huo uliongozwa  rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, huku Idara ya Uhamiaji ikitumia wiki hiyo kutoa Elimu kwa Umma kuhusu masuala ya Uraia,  taratibu za Kupata Pasipoti  na kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya Wahamiaji haramu kuingia nchini ambapo ni hatari kwa ulinzi na Usalama wa Taifa letu.

#Wananchi Fichueni Wahamiaji Haramu

#Jukumu la Ulinzi na Usalama wa Taifa letu ni la kila Mtanzania

 HABARI PICHA NA MATUKIO


Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Marco Gaguti Akiongea na wananchi wa Karagwe hawapo Pichani Wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Sheria

Baadhi ya Maafisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera wakihudumia Wananchi wa Karagwe

Kazi Inaendelea

(Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Kagera)


20 Novemba 2020

DCI Towo Ahitimisha Mafunzo ya Usimamizi wa Masuala ya Ki-Uhamiaji Kwa Taasisi za Umma na Sekta Binafsi.

Moshi, Kilimanjaro

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdallah Towo mapema leo hii amehitimisha  mafunzo ya siku 05 ya usimamizi wa masuala ya Ki-Uhamiaji kwa taasisi za Umma  na sekta binafsi hapa nchini. 

Mafunzo hayo yamefanyika Katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro huku yakihusisha Washiriki wa Kundi la Tisa  (Oparesheni Matokeo).

DCI Towo alieleza kwamba mada zilizofundishwa na kujadiliwa zililenga katika kutafuta njia muafaka ya kuboresha huduma za Ki-uhamiaji.

“Ni wazi kwamba sisi sote tuna wajibu wa kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuweza kufanikisha sera ya taifa ya Tanzania ya Viwanda katika zama hizi za Uchumi wa kati kama inavyosisitizwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli” Alisema DCI Towo

Aidha amempongeza na Kumshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Peter Makakala kwa kuhakikisha kwamba mafunzo haya yanafanyika kama yalivyopangwa na pia kuhakikisha kuwa mafunzo wanayoyapata washiriki yanaleta tija kwa serikali na sekta binafsi kwa ujumla.

Katika Mafunzo hayo ya siku 05 Washiriki walipata fursa ya Kufanya ziara ya Kimafunzo katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), na kupata muda mzuri wa kujifunza mambo kadha wa kadha yahusuyo Mlima huo na mazingira yake.

Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kitaendelea kutoa  ushirikiano wa karibu kwa wadau wote wa sekta binafsi na tasisi za Umma ili kuweza kufanikisha malengo yake na kuhakikisha kuwa wadau wote wanafanya jambo moja lenye kuleta ufanisi na maslahi mapana kwa Ulinzi na Maendeleo ya Taifa letu.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo (Katikati) akiwa katika Picha ya Pomoja Wahitimu wa Mafunzo ya Usimamii wa Masuala ya Ki-Uhamiaji kwa Taasisi na Sekta Binafsi

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mafunzo ya Ki-Uhamiaji Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo akimkabidhi cheti mmoja wa Washiriki wa MafunzoBaadhi ya Wahitimu wa Mafunzo wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Abdalah Towo (hayupo Pichani)


Mkuu wa Itifaki na Uhusiano Kutoka Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA (Kushoto) Mrakibu Msaidizi Leslie Mbotta akitoa maelekezo kwa Timu yake ya Itifaki katika eneo la Hifdhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)


Maafisa, Askari na Wahitimu wa Mafunzo ya Kiuhamiaji wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Lango kuu  la Marangu ambalo hutumika  Kuingilia Katika Kupanda Mlima KilimanjaroMkuu wa Itifaki na Uhusiano Kutoka Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda TRITA (Kushoto) Mrakibu Msaidizi Leslie Mbotta akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Wahitimu wa Mafunzo yya Kiuhamiaji waliowasili katika Hifadhi ya KINAPA  Kwa lengo la KujifunzaBaadhi ya Wahitimu wakiwa katika  Mfano wa Mlima Kilimanjaro
Afisa Utalii Daraja la Kwanza  Herman Mtei kutoka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro  akitoa Maelezo na Historia ya Mlima Kilimanjaro wahitimu wa Mafunzo ya Masuala ya Kiuhamiaji (Hawapo Pichani)

(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

17 Novemba 2020

UHAMIAJI Mtwara Yatoa Mafunzo ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba

Mtwara, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara imetoa Mafunzo ya kiuhamiaji kwa kuruti wa Jeshi la Akiba (Mgambo), Mkoani humo, Jumla ya kuruti 107 wa Jeshi hilo walipatiwa mafunzo hayo ambayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba katika kata ya Raha leo  Wilaya ya Mtwara Mjini huku wakiwa wiki ya  10 ya mafunzo yao ya miezi 03.

Elimu hiyo ilitolewa na Ofisa Kutoka Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara Kitengo cha Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe ambae alifundisha maana ya Uraia, Mhamiaji ni nani na Madhara ya kuwaficha wahamiaji haramu sanjari na kuwafundishwa mbinu za kuwbaini Wahamiaji haramu ikiwemo na kuwakumbusha umuhimu wa wao kushiriki katika  suala zima la ulinzi na usalama wa Taifa.

Katika kuendelea na juhudi hizo za kupambana na changamoto ya Wahamiaji Haramu hapa nchini Idara ya Uhamiaji inaendelea pia kutoa elimu ya Uhamiaji na Uraia kwa Wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mitandao ya kijamii, machapisho, mikutano, na warsha mbalimbali ili kujenga uelewa wa Wananchi juu ya athari za kuwakumbatia wahamiaji haramu.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji kwa Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Mtwara
Kuruti wa Jeshi la Akiba Mkoani Mtwara wakimsikiliza kwa Makini Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Andrew Mwangolombe Akitoa Elimu ya Kiuhamiaji (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mtwara)