Idara ya
Uhamiaji Mkoa wa Iringa mapema wiki hii imekamata wahamiaji Haramu wanne 04
raia wa Somalia na Dereva mmoja (01) raia wa Tanzania wakati wa doria ya
kawaida.
Akithibitisha Taarifa hizo Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Agnes Michael Luziga amesema watuhumiwa wote walikamatwa eneo la Mazombe Wilayani Kilolo na Kikosi Maalumu cha doria cha Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.
Baada ya mahojiano imebainika kuwa watuhumiwa walikuwa wakitokea Mkoani Dar es salaam kama abiria kwenye gari namba T592 DTY aina ya Hiace wakielekea Mkoani Mbeya na baadae Afrika ya Kusini kupitia Malawi, Aliongeza (SACI) Luziga.
Kwa Mjibu wa sheria za Uhamiaji Sura namba 54, Rejeo la Mwaka 2016 pamoja na kanuni zake, Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria na kusafirisha wahamiaji haramu,
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa inaendelea kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano pindi wanapo mtilia shaka mtu yoyote ili kuwezesha kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya Kiuchumi.
![]() |
Watuhumiwa Walioingia Nchini Kinyume cha Sheria |
![]() |
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Agnes Michael Luziga |

![]() |
Gari iliyotumika Kusafirishia Wahamiaji Haramu (Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni