Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

25 Oktoba 2020

Wana HamaHama Bendi yatia fora Tamasha la Amani la Majeshi ya Ulinzi na Usalama

25 Oktoba 2020

Dodoma, Tanzania

Bendi ya Uhamiaji maarufu kama Wana HamaHama Bendi imeshiriki Tamasha la Amani la Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Nyerere jijini Dodoma na kutoa burudani safi kwa wapenzi wa muziki jijini hapa waliofika katika Tamasha hilo  lililoandaliwa na Chama cha muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA)

 

Bendi hiyo ya Uhamiani inayomamiwa na meneja ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Denis Kimaro imeimba nyimbo zinazohamasisha Uzalendo na Amani hasa wakati huu ambapo Taifa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

 

“Bendi yetu imefanya vizuri sana leo maana tumetambulisha nyimbo mpya mbili zinazo hamasisha uzalendo na amani kati ya nyimbo nne tulizoimba, wenzetu wa vyombo vingine vya ulinzi  wameona jinsi gani tulijiandaa kutoa burudani ikizingatiwa kuwa mara yetu ya kwanza kuimba kwenye jukwaa moja na bendi nyingine. Namshukuru Afande CGI kuifufua bendi hii ambayo ilifufa tangu miaka ya 1990, na pia kwa kutuwezesha kuwa na vifaa vya kisasa vya muziki. Aidha tunamshukuru msimamizi mkuu Mrakibu Paul Mselle kwa ushauri na malezi mazuri.Tunaahidi mengi mazuri kutoka kwa Wana Hamahama” alieleza Afisa Uhamiaji huyo mara baada ya Tamasha.

 

Ikumbukwe kwamba, Idara ya Uhamiaji iliwahi kuwa na Bendi iliyotamba miaka ya mwishoni ya 70 hadi mwanzoni mwa 90 baadaye bendi ilikufa na kufufuliwa mwaka 2019 na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dtk. Anna Makakala






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni