Moshi, Kilimanjaro
Mkuu wa chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Ramadhan Towo Mapema leo hii
amefungua mafunzo ya usimamizi wa masuala ya Ki-Uhamiaji kwa taasisi za
serikali na sekta binafsi Katika Ukumbi wa Chuo TRITA-Moshi, Mkoani Kilimanjaro
Akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi DCI Towo amewapongeza washiriki wote kwa kupata bahati kubwa ya kuchaguliwa na taasisi zao kuja kuhudhuria mafunzo muhimu ya masuala ya Ki-Uhamiaji.
“Ni imani yetu kuwa mafunzo mtakayoyapata yatawajenga na kuwandaa ninyi kuwa Mabalozi, viongozi na wasimamizi wazuri wa masuala yote yanayohusu Uhamiaji na Idara ya Kazi, ili kusaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali” Alisema
Idara ya Uhamiaji Tanzania imeweka imani kubwa juu ya washiriki kuwa watapokea mafunzo na kuwa wanafunzi wenye bidii katika kujifunza ili kuongeza tija katika utendaji wa kazi za kila siku hususani zile zinazohusu Uhamiaji na Idara ya Kazi.
“Sisi kama Chuo tunatarajia kwamba mara baada ya kumaliza mafunzo yenu mtakuwa mmeiva na kuongeza ufahamu juu ya musuala ya Ki-Uhamiaji na pia mtakuwa wa wazalendo mliopikwa upya”.
Mafunzo haya yatachukua takribani siku tano, kwa mchanganuo ufuatao Kipindi cha siku Nne Washiriki watakuwa chuoni wakisoma masomo ya darasani, Kipindi kingine cha siku moja, wataenda Day Trip Tour ambayo itakuwa na mafunzo ndani yake.
“Kutokana na tishio la ugonjwa wa Corona tulisitisha mafunzo, lakini hivi karibuni tumeanza tena kutoa mafunzo hayo. Mpaka sasa Ninyi ni kundi la Nane kuhudhuria mafunzo haya, Tunawaomba sana baada ya mafunzo haya mkawe mabalozi wazuri na kutusaidia kualika kampuni na taasisi zingine kuhudhuri mafunzo haya” Alisema DCI Towo.
DCI Towo amewakumbusha washiriki kuendelea kuhudhuria mafunzo hayo mara kwa mara ili kuweza kujengeka na kupata elimu ya kutosha juu ya masuala ya Ki-Uhamiaji.
Chuo
hiki Kilianzishwa mwaka 2007 na kufunguliwa rasmi Disemba 12, 2008 na aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mwaka
2009 Chuo Kilipata usajili baada ya kukidhi viwango vya ubora vya mafunzo
vinavyotambulika na Baraza la Elimu na Ufundi (NACTE) na kupewa namba ya Usajili
REG/PWF/030.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Mkuu wa Itifaki na Uhusiano (TRITA) Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Leslie Mbotta Akiongoza itifaki wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Usimamizi wa Masuala ya Ki-uhamiaji yaliyofanyika Moshi, Kilimanjaro |
![]() |
Mkuu wa chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI) Abdallah Ramadhan Towo (katikati Waliokaa) akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni