Dar es salaam
Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala Mapema leo hii amehudhuria Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi
la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam
Hafla hiyo iliongozwa na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera na Mwenyeji wake Dkt. John
Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Aidha tukio hilo limehudhuriwa pia na Wakuu wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama sanjari na
Mawaziri mbalimbali Makatibu wakuu wa wizara na Viongozi wengine waandamizi wa
serikali bila kuwasahau wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa Ujumla
Kituo hicho cha Mabasi Kitagharimu Zaidi ya Bilioni 70 za Kitanzania ambazo ni fedha za ndani, huku lengo kuu likiwa ni kuwahudumia Wananchi wa Tanzania na Wageni wengine kutoka Nchi Mbalimbali za Jirani na zile za SADC.
HABARI PICHA NA MATUKIO
 |
Muonekano wa Ujenzi wa Kituo Kipya cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam Ukiendelea |
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Akiongea na Wananchi wa Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam |
 |
Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera akiongea na Wananchi wa Dar es salaam wakati wa Uuwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akipokea maelezo ya namna Kituo cha Mabasi Kitakavyokuwa baada ya kuhudhuria Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Jijini Dar es salaam |
 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jaffo akitoa Maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo Kipya cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis |

 |
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Mabasi Mbezi Luis Ujenzi Ukiendelea
|


 |
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Waliohudhuria Hafla hiyo |
 |
Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliohudhuria Hafla hiyo |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akimuaga Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera (Hayupo Pichani) baada ya kumaliza tukio la Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam. |
 |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akimuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumaliza tukio la Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam.
|
 |
Kamishna wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Suleiman Mzee akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya Ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaa |
 |
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi Dkt. John Kijazi (Kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) Balozi Kanali Wilbert Ibunge baada ya Kuhitimisha Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi katika Kituo Kipya cha Mabasi Mbezi Luis Dar es salaam |
 |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni