Dar es salaam
Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala Mapema leo hii amehudhuria Mapokezi ya Ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCatrthy Chakwera kwa ziara rasmi ya siku tatu baada ya kupata Mwaliko kutoka kwa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mapokezi hayo yamefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es salaam na baadae kufanya Mazungumzo katika Ikulu ya Magogoni Dar es salaam.
Katika Mazungumzo yao Rais Dkt. John Magufuli na Rais Dkt. Lazarus McCatrthy Chakwera wamesema miongoni mwa mambo makubwa ambayo Nchi hizi mbili zinaenda Kushirikiana zaidi ni Masuala ya Ki-Uhamiaji ikiwepo kuanzisha vituo vya pamoja mpakani yaani (One Stop Border Post (OSBP) kama zilivyo kwa Tanzania na nchi nyingine ili kuongeza ushirikiano na uhusiano zaidi katika Kufanya Biashara na kuwaletea maendeleo Wananchi wa Tanzania na Malawi.
Ziara ya Rais wa Malawi hapa Nchini ina manufaa Makubwa kwa nchi zote mbili na kufungua ukurasa mpya wa umoja na ushirikiano.
Ziara itaendelea kesho ambapo Rais wa Tanzania na Malawi watashiriki Kuweka Jiwe la Msingi Katika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Kilichopo Mbezi Luis Jijini Dar es salaam.
HABARI PICHA NA MATUKIO
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCatrthy Chakwera akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuwasili Nchini kwa Ziara ya Siku Tatu |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCatrthy Chakwera baada ya Kuwasili Nchini kwa Ziara ya Siku Tatu |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCatrthy Chakwera baada ya kukagua Gwaride la Heshima |
![]() |
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini walipokuwa Wakisubiri Kumpokea Rais wa Malawi |
![]() |
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni