Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

31 Agosti 2020

CGI Dkt. Anna Makakala Aongoza Mamia katika Ibada ya Kumuaga Mhasibu wa Uhamiaji Geofrey Saria Aliyefariki Kwa Ajali.

Dar es salaam, Tanzania

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala ameongoza mamia ya watu katika Ibada takatifu ya kumuaga mtumishi wa Idara ya Uhamiaji aliyekuwa Katika Kitengo cha Uhasibu Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma Marehemu Geofrey Hubert Saria.

Ibada hiyo imefanyika jana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT DMP) Tabata Chang’ombe ambapo ilihudhuriwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, Kamishna wa uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogelo, Kamishna wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga na Kamishna wa Vibali vya Ukaazi Visa na Pasi Mary Palmer (ndc).

Wengine waliohudhuria Ibada hiyo ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi (ACI) Edmund Mrosso Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Mrakibu Paul Mselle Maafisa, Askari na Watumishi  Raia wa Uhamiaji sanjari na ndugu na jamaa wa marehemu Saria.

Akiongea na Maofisa, Askari, Wtumumishi Raia ndugu na jamaa wa Marehemu wakiwemo  Waumini wa KKKT Waliohudhuria Ibada hiyo CGI Dkt. Makakala amesema kwamba  marehemu alikuwa mchapakazi katika kutekeleza majukumu yake kwa utii uhodari na weledi wa hali ya juu wakati wote huku akionesha ushirikiano  na wafanyakazi wenzake.

“Marehemu Saria amefariki katika kipindi ambacho Idara Idara ya Uhamiaji bado inamhitaji sana kwa mchango wake katika Kulitumikia Taifa” alisema CGI Dkt. Makakala

Akisoma Wasifu wa Marehemu Mrakibu wa Uhamiaji Andrew Malyeta alisema Marehemu Geofrey Saria alizaliwa  25 Octoba 1989 katika Hospitali ya Mikocheni katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Mwaka 1997 Marehemu alipata Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Tabata Relini iliyoko Jijini Dar e salaam na kuhitimu mwaka 2003, Mnamo mwaka 2004 alijiunga na Shule ya Sekondari Makongo iliyoko Jijini Dar es salaam na Kuhitimu  kidato cha nne mwaka 2007.

Aidha mwaka 2008 alirudi tena katika shule ya Sekondari Makongo kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita na kuhitimu mwaka 2010, mwaka 2011 marehemu alijiunga na chuo cha Uhasibu Arusha kwa Masomo ya Elimu ya Juu na mwaka 2013 alihitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Uhasibu.

Mwaka 2014 Marehemu alifanya Mtihani wa Uhasibu na Kutunukiwa cheti cha juu cha Uhasibu CPA (T) na Bodi ya Taifa ya Uhasibu Tanzania (NBAA).

Marehemu Saria Aliajiriwa serikalini katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ndani ya Idara ya Uhamiaji kuanzia tarehe 01 Septemba 2015 akiwa Mhasibu daraja la II na alipangiwa Kituo cha Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dar e s salaam.

Mnamo Tarehe 19 Oktoba  Marehemu alihamishwa kutoka katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es salaam na kuhamia Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dodoma, kufuatia uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma.

Mpaka umauti unamkuta marehemu alikuwa akihudumu katika Ofisi za Uhamiaji Makao Makuu Dodoma Kitengo cha Uhasibu.

Marehemu alifariki siku Jumapili ya tarehe 23 Agosti mwaka huu 2020 kwa ajali ya gari iliyotokea Mkoani Morogoro  alipokuwa safarini kutka Dar es salaam kuelekea Dodoma

Marehemu alizaliwa 25 Ocktoba 1989 na Kufariki Tarehe 23 Agosti 2020 kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Dar es salaam.

HABARI PICHA NA MATUKIO
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa salamu za mwisho kwa marehemu Geofrey Saria

Mwili wa Marehemu ukiwasili Kanisani


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiteta jambo na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Chogelo

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiteta jambo na Kamishna wa Urai na Pasipoti Gerald Kihinga

Mtunza Nidhamu wa Idara ya Uhamiaji RSM Zahara Akida akifuatilia kwa Makini Mahubiri katika Ibada ya Kumuaga marehemu Geofrey Saria katika Kanisa la KKKT DMP Usharika wa Tabata





Kamishna wa Uhamiaji Divisheni ya Vibali vya Ukaazi Pasi na Visa Mary Plmer (Ndc) Kulia akiteta jambo na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Edmund Mrosso wakati wa Ibada ya Kuuaga Mwili wa Marehemu Geofrey Saria

Pichani wa Kwanza Kulia ni Mama Mzazi wa Geofrey Saria akiwa katika Ibada ya Kumuaga Mwanae katika Kanisa la KKKT Tabata

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akitoa salamu za rambi rambi wakati wa ibada ya Kumuaga Marehemu Geofrey Saria







Familia ya Marehemu Geofrey Saria Ikitoa Salamu zao za Mwisho



Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mrosso akitoa salamu za mwisho kwa marehemu Geofrey Saria


Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzani Mrakibu Paul Mselle Akitoa Salamu za Mwisho kwa Marehemu Geofrey Saria



Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika msibani



Makaburini





Makamishna wa Uhamiaji wakiweka shada la Maua





Mama Mzazi wa Marehemu na ndugu wa Karibu wakiweka Shada la maua















Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mchungaji wa KKKT DMP Usharika wa Tabata aliyeongoza Ibada ya kumuaga Marehemu Geofrey Saria


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akimpa pole na kuagana na Mama Mzazi wa Marehemu Geofrey Saria






Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala akiagana na Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha (CI) Edward Chogelo


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiondoka mara baada ya Kuhudhuria Ibada Takataifu na Mazishi ya Marehemu Geofrey Saria (Picha Zote na Kitengo cha Uhusiano
Uhamiaji Makao Makuu)