Mwanga, Kilimanjaro
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala ameipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya
Mwanga Mkoani Kilimanjaro inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Thomas Cornel
Apson kwa juhudi na mpango mkakati walionao wa kutokomeza wahamiaji haramu
wilayani humo.
Ameyasema hayo wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya mipaka na utendaji kazi kwa maofisa
na askari wa Uhamiaji nchini.
Akiwa katika ukaguzi
wa kipenyo cha Kitobo, Kitoghoto na Mkisha Wilayani Mwanga CGI Dkt. Anna Makakala
amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro
na Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Mwanga kwani wamehamasisha ulinzi shirikishi wa
mipaka katika maeneo hayo kwa kushirikiana na wananchi na wadau Mbalimbali.
Aidha amelishukuru
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini (Red Cross) Mkoa wa Kilimanjaro kwa kusaidia
kutoa baadhi ya vifaa vya kusaidia ulinzi katika vipenyo vya Kighoto ambapo
wametoa Mahema (Tents) 02 ambayo hutumika na askari wa Uhamiaji na askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) wanaojitolea kulinda baadhi ya maeneo korofi yanayosadikika kupitisha
wahamiaji haramu katika Wilaya hiyo sanjari na kutoa jozi 02 za sare za Askari
wa Jeshi la Akiba.
Mkuu wa Wilaya Mwanga
Mhe. Thomas Apson Akiongea na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt.
Anna Makakala ofsini kwake amempongeza kwa utendaji kazi wake na uhodari katika
kuiongoza vyema Idara ya Uhamiaji Kwa mafanikio makubwa.
Mhe. Apson ameomba
kuweza kuongezewa nguvu ya askari katika wilaya yake ili kuongeza kasi ya kudhibiti
kabisa wa wahamiaji haramu, kwani katika Wilaya hiyo kuna maeneo mengi ya vipenyo
vya kupitisha wahamiaji haramu kutokana na Jiografia ya wilaya hiyo kwa asilimia
kubwa kupakana na nchi ya Kenya ambapo Wahamiaji haramu wengi hutumia maeneo
hayo kuingia nchini Kinyume cha sheria.
Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Tununasya Ng’ondya alieleza
kwamba baada ya kuona changamoto kubwa ya uingiaji wa Wahamiaji Haramu Wilayani
Mwanga alishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wilaya ya
Mwanga ambapo kupitia Mshauri wa Mgambo Mkoa na Wilaya ya Mwanga walianzisha
mafunzo ya Mgambo katika kata za mpakani, ambao sasa askari hao wanajitolea kwa uzalendo katika
kuongeza nguvu ya ulinzi wa mipaka ya nchi yetu kwa utii, uhodari na weledi wa hali
ya juu huku wakishirikiana kwa karibu sana na Maofisa na Askari wa Uhamiaji
Wilayani hapo.
Akitoa taarifa fupi
ya Utendaji kazi ya Wilaya ya Mwanga Afisa Uhamiaji (W) Mrakibu Lydia Moshi
alisema Wanashirikiana vyema na kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na
wananchi kwa ujumla katika mapambano dhidi ya Wahamiaji Haramu, ikiwemo utoaji wa elimu kwa umma juu ya madhara ya Wahamiaji haramu.
Kutokana na kuwa na
uhusiano wa karibu na wadau mbalimbali Ofisi ya Uhamiaji Wilaya na Mkoa
walitafuta wadau na kuwapata baadhi yao wakiwemo Shirika la Msalaba Mwekundu
(Red Cross) Mkoa wa Kilimanjaro ambao nao wamekuwa msaada mkubwa katika
kuchangia kupambana na wahamiaji haramu kwani wamesaidia kutoa vifaa mbalimbali
kama vile Mahema (Tents) 02 katika maeneo ya Kitobo na Kivisini kwa maana ya
kulinda kipenyo cha majini katika Ziwa Jipe na eneo la Kitoghoto.
Ziara ya CGI Dkt.
Anna Makakala ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi na baada ya kumaliza Wilayani Mwanga, aliendelea tena Mkoani Kilimanjaro na kukagua maeneo ya mipaka iliyopo
Wilaya ya Rombo ikiwemo Tarakea, Holili na Rongai na baadae kuongea na Maafisa
na Askari wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro.
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Mwanga Mhe. Thomas Cornel Apson alipowasili Wilayani Hapo kwa ziara ya Kikazi |
![]() |

![]() |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitoghoto Bw. Ayubu Ramadhan akionesha Hema (Halupo Pichani) walilopokea kutoka katika Shirika la Msalaba Mwekundu Mkoa wa Kilimanjaro |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akipokea maelezo ya Moja ya Beacon Ndogo inayotenganisha mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania uliopo Wilayani Mwanga |
![]() |
Moja ya Sehemu ambayo wahamiaji haramu walikuwa wanatumia kuingia nchini kinyume na Sheria sasa Imedhibitiwa |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiangalia baadhi ya Mitumbwi iliyokuwa ikitumika kuvushia wahamiaji Haramu katika kijiji cha Mkisha kilichopo kata ya Jipe Wilayani Mwanga |
![]() |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akiongea na Wanchi wa Kijiji cha Mkisha kilichopo Kata ya Jipe Wilayani Mwanga |
![]() |
Mmoja wa Wazee Maarufu wa Kijiji cha Mkisha akieleza Changamoto wanazozipata katika eneo hilo |
![]() |
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania CGI Dkt. Anna Makakala akiwasihi wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ili kukomesha kabisa wimbi la wahamiaji haramu hapa nchini |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni