Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Januari 2021

UHAMIAJI Tanzania Yapokea Pikipiki Kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji

Dodoma, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Tanzania mapema leo hii imepokea pikipiki 04 kutoka shirika la kimataifa la Uhamiaji ikiwa ni mchango mojawapo wa miradi yenye malengo ya kuongeza uwezo wa vitengo vya doria mpakani kwenye idara na kusimamia uhamiaji haramu. 

Akipokea pikipiki hizo katika ofisi ya makao makuu ya Uhamiaji Dodoma, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala amelishukuru shirika hilo kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia Idara ya uhamiaji kutekeleza majukumu yake hasa katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

CGI Dkt. Makakala amesema kwamba pikipiki hizo zimefika wakati muafaka na zitaenda kusaidia zaidi mipakani ili kuimarisha doria na misako kwani Uhamiaji holela unapaswa kupingwa, kwa sababu ni hatari na mbaya kwa usalama wa taifa.

Aidha ameliomba shirika hilo kuendelea kushirikiana zaidi katika shughuli zake zingine zikiwemo za kusaidia vifaa muhimu vinavyohitajika katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma kichakamiba iliyopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.

Kwa upande wake Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi akitoa maelezo ya awali ya mchango wa pikipiki katika Idara ya Huduma za Uhamiaji alisema amefurahi sana kushiriki na kuiwakilisha IOM katika shughuli hiyo muhimu ya kukabidhi pikipiki kwa Idara ya Uhamiaji.

“Wengi wenu mtakuwa mnafahamu kwamba, mwaka jana Julai 2020 Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM), Shirika la Uhamaji la Umoja wa Mataifa (UN) lilitoa pikipiki tano za Honda XL125 na leo tarehe 28 Januari 2021, linafuraha kutoa Honda 4 zaidi aina ya XL125 katika Idara ya Huduma za Uhamiaji” alisema Dr Qasim Sufi

Mchango huu muhimu (wenye thamani ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano 25,000) unatolewa na IOM chini ya Mradi wa Uhamaji wa ukanda wa Afrika – ikiwa ni awamu ya 10 katika Ukanda wa Mashariki na Pembe ya Afrika ulioyofadhiliwa na Idara ya Serikali Ofisi ya watu, Wakimbizi na Uhamiaji (BPRM) wa Nchini Marekani (USA)

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akipokea pikipiki kutoka kwa Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Pikipiki zilizokabidhiwa 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akisaini hati ya makabidhiano ya pikipiki katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala na Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi wakionesha hati za makabidhiano ya pikipiki 04 katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

26 Januari 2021

UHAMIAJI IRINGA YASHIRIKI MAONESHO YA UWEKEZAJI

 Iringa, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa imeshiriki maonesho ya mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Iringa, Maonesho hayo yalifunguliwa tarehe 23 January 2021 na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) katika viwanja vya maonesho vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE).

Katika maonesho hayo yaliyodumu kwa siku mbili huduma mbalimbali za ki-uhamiaji zilitolewa kama vile ukaguzi na upitishaji wa fomu za vitambulisho vya taifa, elimu ya uraia, elimu juu ya uhamiaji haramu na madhara yake kwa jamii na taifa kwa ujumla sanjari na  kupokea maombi ya passipoti ya kielektroniki n.k.

Maonesho hayo yalijumuisha taasisi za uuma na binafsi zinazotoa huduma katika Mkoa wa Iringa.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Elimu ikitolewa

(Picha zote na kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa)

18 Januari 2021

Waziri Simbachawene afungua mafunzo ya kozi ya uongozi kwa Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba Tanga. 

Tanga, Tanzania 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene ameongoza hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya uongozi kwa maafisa na askari wa Uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba iliyopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.

Mhe. Simbachawene amempongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, maafisa na askari wa Uhamiaji kwa kuwa na moyo wa uzalendo wa kuanzisha kambi hiyo ya mafunzo kwa kuanza na  kuchangia wenyewe kwa hiari gharama za ujenzi wa awali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala inaeleza kwamba ujenzi wa kambi hiyo ulianza rasmi mwezi Julai, 2020 na kiasi kilichotumika ni shilingi milioni 140, fedha hizo zimetokana na michango ya hiari ya askari na maafisa wa Uhamiaji ambao walichangia Shilingi milioni 81 na wadau rafiki wa uhamiaji walichangia milioni 59 ikiwemo vifaa vya ujenzi.

Aidha, Mhe. Simbachawene aliwataka wanafunzi wa Kambi hiyo kuzingatia masomo ya Ki-uhamiaji wanayopewa yakiwemo ya uongozi na utawala, masuala ya kikonsula, mawasiliano, ulinzi wa kujihami na gwaride.

"Mafunzo mtakayoyapata kutoka kwa wakufunzi wenu yanalenga kudumisha nidhamu ya kijeshi, uzalendo, utii, uwajibikaji na maadili bora, ninawaomba zingatieni tunu hizo katika kipindi hiki chote cha mafunzo, kwani ndio silaha kubwa kwa askari na katika uongozi bora," alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, alisema mafunzo katika kambi hiyo mpya, yanajumuisha jumla ya askari na maafisa wa uhamiaji 287, wanawake 81 na wanaume 206, ambapo mchanganuo wa kozi ya Mrakibu Msaidizi wapo 32, Mkaguzi Msaidizi wapo 112, kozi ya Sajini 42 na kozi ya Koplo wapo 101.

"Mheshimiwa mgeni rasmi napenda kukujulisha kuwa Kambi ya Mafunzo ya Boma Kichaka Miba inamilikiwa na Idara ya Uhamiaji na Chuo cha Kikanda (TRITA) kilichopo Mjini Moshi,  Ujenzi wa Kambi hii ulianza rasmi mwezi Julai, 2020 huku ikiwa na ukubwa wa ekari 395 na tayari tumekabidhiwa hati miliki” alisema Dkt. Makakala.

Aliongeza kwamba lengo la kuanzishwa kwa kambi hiyo ya mafunzo ni kukidhi mahitaji ya Idara kwa kutoa mafunzo ya utayari kwa wakati ili kuweza kupata askari wakakamavu, wenye nidhamu, weledi na maadili ya kazi za Ki-uhamiaji.

Hapo awali Kutokana na Idara kutokuwa na kambi yake ya mafunzo, ilipelekea kuanza mafunzo nje ya muda uliopangwa, kuendesha mafunzo kwa gharama za juu pamoja na kukosekana kwa utamaduni wa kiutendaji wa taasisi (Organization culture) ili kukidhi malengo ya Idara, Kwani askari walikua wakipata uzoefu tofauti tofauti kutoka vyuo vya Taasisi zingine. 

Manufaa yatokanayo na uanzishwaji wa Kambi hii ni pamoja na; kuongeza uwezo katika kuzuia na kudhibiti wahamiaji haramu hapa nchini hususan katika mikoa ya mpakani na nchi jirani ikiwemo Tanga, Pwani (Bagamoyo) na Kilimanjaro.

Pia kambi hii itasaidia kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa kuipatia Idara ya Uhamiaji utaalamu wa kupambana na makosa mbali mbali yakiwemo yale yanayovuka mipaka (Transnational Organized Crimes). 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akitoa salamu za Mkoa aliwataka wananchi waishio jirani na kambi hiyo kutoa ushirikiano na kambi hiyo, na pia wasivamie maeneo ya kambi hiyo ya Uhamiaji wakaona vichaka wakafikiri ni eneo ambalo halina mwenyewe na wakavamia.

Aidha amemshukuru CGI Dkt. Anna Makakala kwa uamuzi wake, ujasiri na weledi wa hali ya juu kwa kuona umuhimu wa kuliendeleza eneo hili ambapo ni zaidi ya miaka 17 tangu linamilikiwa na Uhamiaji.

“Ni awamu hii katika uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli umeweza kuwa na viongozi makini, hodari na wenye weledi wa hali ya juu wanaoweza kuanzisha kambi hii, hongera sana CGI Dkt. Makakala, sisi wana Tanga tunafarijika sana kwa sababu unatuweka kwenye ramani nzuri na tutapata mafanikio makubwa kwani uchumi wetu utachangamka na kuongezeka hivyo niwaombe wanachi wa Mkinga na Tanga kwa Ujumla kuchangamkia fursa” alisema Mhe. Shigela

HABARI PICHA NA MATUKIO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akibadilishana machache na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na makamishna wa Uhamiaji kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Tanga kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mkinga kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi a wananchi na viongozi wa kijiji cha Boma kichakamiba wilayani Mkinga, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa koi ya uongozi katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba Tanga, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na askari wanafunzi, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba TangaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akiongea na mmoja wa kiongozi wa kijiji cha Boma Kichakamiba

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akitoa hotuba ya ufunguzi wa kozi ya kwanza ya uongozi katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji


 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akitoa maelezo mafupi ya ufunguzi wa kozi ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akitoa salamu za Mkoa wakati wa ufunguzi wa kozi ya kwanza ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji


Msemaji mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle akiongoza itifaki za hafla ya ufunguzi  wa kozi ya kwanza ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba Tanga
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba TangaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akiweka jiwe la mingi la ujenzi wa jengo la Utawala katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga

Mtaalamu wa majengo Uhamiaji makao makuu Konstebo Denis Assey akitoa maelezo ya ujenzi wa kambi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene  katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na viongozi wa ccm Mkoa wa Tanga na Wilaya ya Mkinga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akisalimina na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela

Ujenzi wa jengo la Utawala ukiendelea  katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga 


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Mkinga Mhe. Mark Yona
Muonekano wa jengo la utawala kwa nyuma litakapokamilika

Muonekano wa jengo la utawala kwa mbele litakapokamilika 


(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)