Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

15 Januari 2021

Zoezi la kuandikisha walowezi lazinduliwa rasmi Tanga.

Tanga, Tanzania

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Mark Yona mapema wiki hii amezindua zoezi la uandikishaji walowezi nchini lililofanyika Mkoani Tanga Wilayani Mkinga katika Kata ya Duga mpakani na nchi ya jirani Kenya.

Mhe. Yona alisema Wilaya ya Mkinga ndio inaongoza kuwa na walowezi wengi takriban  elfu 12 kutokana na muingiliano mkubwa na nchi jirani ya Kenya ikichangiwa shughuli za kilimo cha mkonge.

Mkoa wa Tanga una historia kubwa ya kupokea wahamiaji tangu wakati wa ukoloni kwani wapo waliotoka katika mataifa ya Msumbiji, Burundi, Kongo DRC ambayo hayapakani na Mkoa wa Tanga. Wahamiaji hao walikuja kufanya kazi katika mahamba ya Mkonge kama Manamba. Aidha wapo pia wahamiaji kutoka nchi ya jirani ya Kenya ambao wengi wao wapo katika Wilaya yetu ya Mkinga.  

“Tumepata hii nafasi ya kuwa wa kwanza kutambuliwa na kuandikishwa tuitumie vizuri fursa hiyo kwa kujitokeze kwa wingi kujiandikisha ili kuweza kutambuliwa na kupata fursa zinatolewa na Srerikali kama vile kusajili laini zenu za simu na kupata vitambulisho vya Taifa kama wageni,  badala ya kutumia laini za simu zilizosajiliwa na watu wengine. Pia itakusaidia kukaaa na kuishi kwa amani bila kujificha ficha .”alisema Mhe. Yona

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima alihudhuria shughuli hizo na kusema kwamba zoezi hilo lina manufaa kwa walowezi watakaojiandikisha kwani Serikali ya awamu ya tano itajitaidi kuhakikisha linafanikiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuwatambua wageni wote wanaoshi nchini bila kuwa na hadhi ya Kiuhamiaji.

Aidha amewataka wananchi, kupeana taarifa huko wanapoishi na katika nyumba za ibada ili zoezi liwe lenye matokeo chanya na  manufaa kwa wote.

Bw. Kailima alibainisha kwamba baada ya zoezi hilo kuisha hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuwa sio raia wa Tanzania na Wanaishi hapa nchini bila ya kuwa na hadhi yoyote ya ki-uhamiaji.

Kwa upande wake mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini, Kamishna  wa Uhamiaji divisheni ya uraia na pasipoti Gerald Kihinga alisema zoezi hilo halina lengo la kuwaondosha walowezi nchini  bali Idara inakusudia kuwatambua wahamiaji wote wanaoishi nchini na kuwapatia hadhi za ki-uhamiaji kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mwakilishi wa IOM nchini Dkt. Qasim Sufi alisema Shirika la Uhamiaji Duniani kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji na ufadhili wa UKAid watafanya zoezi hilo kwa kuanza na  Mikoa 11 ambayo ina tatizo la walowezi. Aidha wapo ambao waliosajiliwa kipindi cha nyuma na wengine bado, hivyo kwa zoezi la sasa wanagetemea wahamiaji wengi zaidi watasajiliwa ili kuwapatia hadhi ya ki-uamiaji.

HABARI PICHA NA MATUKIO

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoana na DC Mkinga Mhe. Yona Mark akipata maelezo  jinsi wananchi wanavyoajiliwa kwa mfumo wa kisasa kutoka kwa Mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji Henericus Kanyaruju

Wananchi wa kijiji cha Duga  waliohudhuria  zoezi la ufunguzi a uandikishaji  wa walowezi
Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Bw. Ramadhan Kailima akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Mkinga katika Kijiji cha Duga kuhusu umuhimu wa zoezi la kuandikisha walowezi 



(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni