Waziri Simbachawene afungua mafunzo ya kozi ya uongozi
kwa Maafisa na Askari wa Uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba
Tanga.
Tanga, Tanzania
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene ameongoza hafla ya ufunguzi
wa mafunzo ya uongozi kwa maafisa na askari wa Uhamiaji katika kambi mpya ya
mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba iliyopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.
Mhe.
Simbachawene amempongeza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna
Makakala, maafisa na askari wa Uhamiaji kwa kuwa na moyo wa uzalendo wa
kuanzisha kambi hiyo ya mafunzo kwa kuanza na kuchangia wenyewe kwa hiari gharama za ujenzi
wa awali.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Makakala
inaeleza kwamba ujenzi wa kambi hiyo ulianza rasmi mwezi Julai, 2020 na kiasi
kilichotumika ni shilingi milioni 140, fedha hizo zimetokana na michango ya
hiari ya askari na maafisa wa Uhamiaji ambao walichangia Shilingi milioni 81 na
wadau rafiki wa uhamiaji walichangia milioni 59 ikiwemo vifaa vya ujenzi.
Aidha, Mhe.
Simbachawene aliwataka wanafunzi wa Kambi hiyo kuzingatia masomo ya Ki-uhamiaji
wanayopewa yakiwemo ya uongozi na utawala, masuala ya kikonsula, mawasiliano,
ulinzi wa kujihami na gwaride.
"Mafunzo
mtakayoyapata kutoka kwa wakufunzi wenu yanalenga kudumisha nidhamu ya kijeshi,
uzalendo, utii, uwajibikaji na maadili bora, ninawaomba zingatieni tunu hizo
katika kipindi hiki chote cha mafunzo, kwani ndio silaha kubwa kwa askari na
katika uongozi bora," alisema Simbachawene.
Kwa
upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, alisema
mafunzo katika kambi hiyo mpya, yanajumuisha jumla ya askari na maafisa wa
uhamiaji 287, wanawake 81 na wanaume 206, ambapo mchanganuo wa kozi ya Mrakibu
Msaidizi wapo 32, Mkaguzi Msaidizi wapo 112, kozi ya Sajini 42 na kozi ya Koplo
wapo 101.
"Mheshimiwa
mgeni rasmi napenda kukujulisha kuwa Kambi ya Mafunzo ya Boma Kichaka Miba
inamilikiwa na Idara ya Uhamiaji na Chuo cha Kikanda (TRITA) kilichopo Mjini
Moshi, Ujenzi wa Kambi hii ulianza rasmi
mwezi Julai, 2020 huku ikiwa na
ukubwa wa ekari 395 na tayari tumekabidhiwa hati miliki” alisema Dkt. Makakala.
Aliongeza
kwamba lengo la kuanzishwa kwa kambi hiyo ya mafunzo ni kukidhi mahitaji ya
Idara kwa kutoa mafunzo ya utayari kwa wakati ili kuweza kupata askari
wakakamavu, wenye nidhamu, weledi na maadili ya kazi za Ki-uhamiaji.
Hapo
awali Kutokana na Idara kutokuwa na kambi yake ya mafunzo, ilipelekea kuanza
mafunzo nje ya muda uliopangwa, kuendesha mafunzo kwa gharama za juu pamoja na
kukosekana kwa utamaduni wa kiutendaji wa taasisi (Organization culture)
ili kukidhi malengo ya Idara, Kwani askari walikua wakipata uzoefu tofauti
tofauti kutoka vyuo vya Taasisi zingine.
Manufaa
yatokanayo na uanzishwaji wa Kambi hii ni pamoja na; kuongeza uwezo katika
kuzuia na kudhibiti wahamiaji haramu hapa nchini hususan katika mikoa ya
mpakani na nchi jirani ikiwemo Tanga, Pwani (Bagamoyo) na Kilimanjaro.
Pia kambi
hii itasaidia kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa kuipatia Idara ya Uhamiaji
utaalamu wa kupambana na makosa mbali mbali yakiwemo yale yanayovuka mipaka (Transnational
Organized Crimes).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akitoa salamu za Mkoa aliwataka wananchi waishio jirani
na kambi hiyo kutoa ushirikiano na kambi hiyo, na pia wasivamie maeneo ya kambi
hiyo ya Uhamiaji wakaona vichaka wakafikiri ni eneo ambalo halina mwenyewe na
wakavamia.
Aidha amemshukuru CGI Dkt. Anna Makakala kwa uamuzi wake, ujasiri na weledi wa hali ya juu kwa kuona umuhimu wa kuliendeleza eneo hili ambapo ni zaidi ya miaka 17 tangu linamilikiwa na Uhamiaji.
“Ni awamu hii katika uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli umeweza kuwa na viongozi makini, hodari na wenye weledi wa hali ya juu wanaoweza kuanzisha kambi hii, hongera sana CGI Dkt. Makakala, sisi wana Tanga tunafarijika sana kwa sababu unatuweka kwenye ramani nzuri na tutapata mafanikio makubwa kwani uchumi wetu utachangamka na kuongezeka hivyo niwaombe wanachi wa Mkinga na Tanga kwa Ujumla kuchangamkia fursa” alisema Mhe. Shigela
HABARI PICHA NA MATUKIO
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akibadilishana machache na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na makamishna wa Uhamiaji kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Tanga kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mkinga kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi a wananchi na viongozi wa kijiji cha Boma kichakamiba wilayani Mkinga, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa koi ya uongozi katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba Tanga, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na askari wanafunzi, kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akiongea na mmoja wa kiongozi wa kijiji cha Boma Kichakamiba |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akitoa hotuba ya ufunguzi wa kozi ya kwanza ya uongozi katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akitoa maelezo mafupi ya ufunguzi wa kozi ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akitoa salamu za Mkoa wakati wa ufunguzi wa kozi ya kwanza ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji
|
|
Msemaji mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu Paul Mselle akiongoza itifaki za hafla ya ufunguzi wa kozi ya kwanza ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo Boma Kichakamiba Tanga |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akiweka jiwe la mingi la ujenzi wa jengo la Utawala katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga |
|
Mtaalamu wa majengo Uhamiaji makao makuu Konstebo Denis Assey akitoa maelezo ya ujenzi wa kambi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na viongozi wa ccm Mkoa wa Tanga na Wilaya ya Mkinga |
|
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akisalimina na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela |
|
Ujenzi wa jengo la Utawala ukiendelea katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba Tanga |
|
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini CGI Dkt. Anna Makakala akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Mkinga Mhe. Mark Yona |
|
Muonekano wa jengo la utawala kwa nyuma litakapokamilika |
|
Muonekano wa jengo la utawala kwa mbele litakapokamilika |
|
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni