Visitors

IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA UHAMIAJI HABARI BLOGU KARIBU KWENYE BLOG RASMI YA IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA TUNAKULETEA MATUKIO YANAYOTOKEA KILA SIKU KATIKA IDARA YA UHAMIAJI TAFADHALI TUNAOMBA TUFUATILIE PIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

28 Januari 2021

UHAMIAJI Tanzania Yapokea Pikipiki Kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji

Dodoma, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Tanzania mapema leo hii imepokea pikipiki 04 kutoka shirika la kimataifa la Uhamiaji ikiwa ni mchango mojawapo wa miradi yenye malengo ya kuongeza uwezo wa vitengo vya doria mpakani kwenye idara na kusimamia uhamiaji haramu. 

Akipokea pikipiki hizo katika ofisi ya makao makuu ya Uhamiaji Dodoma, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala amelishukuru shirika hilo kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia Idara ya uhamiaji kutekeleza majukumu yake hasa katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

CGI Dkt. Makakala amesema kwamba pikipiki hizo zimefika wakati muafaka na zitaenda kusaidia zaidi mipakani ili kuimarisha doria na misako kwani Uhamiaji holela unapaswa kupingwa, kwa sababu ni hatari na mbaya kwa usalama wa taifa.

Aidha ameliomba shirika hilo kuendelea kushirikiana zaidi katika shughuli zake zingine zikiwemo za kusaidia vifaa muhimu vinavyohitajika katika kambi mpya ya mafunzo ya Uhamiaji Boma kichakamiba iliyopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.

Kwa upande wake Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi akitoa maelezo ya awali ya mchango wa pikipiki katika Idara ya Huduma za Uhamiaji alisema amefurahi sana kushiriki na kuiwakilisha IOM katika shughuli hiyo muhimu ya kukabidhi pikipiki kwa Idara ya Uhamiaji.

“Wengi wenu mtakuwa mnafahamu kwamba, mwaka jana Julai 2020 Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM), Shirika la Uhamaji la Umoja wa Mataifa (UN) lilitoa pikipiki tano za Honda XL125 na leo tarehe 28 Januari 2021, linafuraha kutoa Honda 4 zaidi aina ya XL125 katika Idara ya Huduma za Uhamiaji” alisema Dr Qasim Sufi

Mchango huu muhimu (wenye thamani ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano 25,000) unatolewa na IOM chini ya Mradi wa Uhamaji wa ukanda wa Afrika – ikiwa ni awamu ya 10 katika Ukanda wa Mashariki na Pembe ya Afrika ulioyofadhiliwa na Idara ya Serikali Ofisi ya watu, Wakimbizi na Uhamiaji (BPRM) wa Nchini Marekani (USA)

HABARI PICHA NA MATUKIO

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akipokea pikipiki kutoka kwa Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Pikipiki zilizokabidhiwa 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala akisaini hati ya makabidhiano ya pikipiki katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala na Katibu Mkaazi wa IOM, Dr Qasim Sufi wakionesha hati za makabidhiano ya pikipiki 04 katika ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma
(Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni