Iringa, Tanzania
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa imeshiriki maonesho ya mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Iringa, Maonesho hayo yalifunguliwa tarehe 23 January 2021 na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) katika viwanja vya maonesho vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE).
Katika maonesho hayo yaliyodumu kwa siku mbili huduma mbalimbali za ki-uhamiaji zilitolewa kama vile ukaguzi na upitishaji wa fomu za vitambulisho vya taifa, elimu ya uraia, elimu juu ya uhamiaji haramu na madhara yake kwa jamii na taifa kwa ujumla sanjari na kupokea maombi ya passipoti ya kielektroniki n.k.
Maonesho hayo yalijumuisha taasisi za uuma na binafsi zinazotoa huduma katika Mkoa wa Iringa.
HABARI PICHA NA MATUKIO
(Picha zote na kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Iringa) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni